CLEVER WEB TZ

Breaking News
Loading…

Pages

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
ENEZA BIASHARA YAKO

Friday, January 31, 2020

DEREVA TOYO 13

Dereva toyo Mtunzi:Richard Yassin Sehemu ya 13 Na kunipaisha katika maisha.Nilimuondoa hofu kuwa ushauri wake ungefanyiwa kazi kwa hiyo asiwe na wasiwasi kuhusiana na mimi.Hivyo mara baada ya kukata simu hiyo ghafla nilisikia hodi ikigongwa mlangoni kwangu.Nilikwenda kufungua mlango ila cha ajabu nilishangaa kumuona tena ma Abasi."Mama unataka nini tena kwangu?Si unajua majirani zetu."Nilimhoji mama huyo ila hakunijibu zaidi ya kunisukuma na kuingia ndani chumbani.Sikuwa na suala jingine la kufanya zaidi ya kuchungulia nje kuona kama kuna jirani aliyekuwa akichungulia na nilipoona kweupe niliingia ndani na kufunga mlango barabara. "Sasa ndugu yangu huogopi wenzako wakikuona alafu kumbuka wewe ni mke wa mtu."Nilimhoji mama huyo ambaye alinitazama kwa jicho kali. "Kwa hiyo hunitaki au nisemeje?Mimi ndo nishapenda kwani siwezi vumilia kuwa na mtu ambaye yuko mbali.Yule atabaki kuwa mume kwa jina ila wewe ni mume kwa vitendo.Maana mimi ni binadamu na nina hisia.Nahitaji kupata faraja kama wanazopata wanawake wengine.Na siwezi kukaa kama gogo tu nikimngoja." Kauli hiyo ilinifanya nizidi kuchanganyikiwa na kujihoji mwenyewe akilini mwangu." Huyu mama ameonja asali na anataka kuchonga mzinga.Na je nitafanyaje dhidi ya mtego huu wa wake za watu?Ukizingatia Angel ameolewa na niko naye kimapenzi naye anamlalamikia mumewe.Ma Abasi naye ndo vilevile.Ila ngoja nikomaze akili kwani uwepo wa majaribu haya ni kukomaa kwa akili.Potelea mbali nitayaweza." Nilimuonyesha ishara ya kuja kitandani ili niweze kumpa mambo aliyoyahitaji.Naye bila hiyana alikuja.Nilimuangalia nimuanze ki vp kwani nilishtukiziwa kufanya jambo ambalo sikuwa nimelipanga.Ila kama waswahili wanavyosema mwanaume mashine.Nilimvuta karibu na.....Itaendelea!!!

Friday, January 17, 2020

TYPHIN 11

TYPHIN 11
‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
“binti yangu, umeipata wapi roho ya kikatili kama hiyo?” Mohammed aliuliza na kumfanya Rabia aone aibu na kutazama chini.
Mwendo wa kuifuata barabara ukfikia kwenye kona, na baadae kwenye mzunguko na kuwajulisha kuwa wameshafika kwenye geti la kuingilia hospitali ya Muhimbili. Walichukua kadi ndogo kwa mlinzi na kuifuata gari ya polisi hadi sehemu ya wodi ya wagonjwa mahututi. Binti huyo akapokelewa, lilipohitajika jina moja kwa mtu aliye karibu naye, Samira alikubali liandikwe jina lake.
Watu wa huduma ya kwanza waliwahi na kitanda. Haraka akawahishwa wodini katika harakati za kuyapigania maisha yake.
**************
Daktari alitoka akiwa na karatasi mkononi, akaita jina la mgonjwa. Inspekta Salim alienda kwa daktari akiongozana na Salehe.
“majibu ya X - Ray yanasema hajavunjika popote. Hivyo nimeandika hapa dawa za kutuliza maumivu. Utapita hapo dirishani na kuchukua.”
Yalikua majibu mazuri yaliyotoa tabasamu kwa wote wawili. Walipita dirishani na kuchukua dawa. Baada ya hapo Inspekta Salim akaenda kwenye mgahawa mmoja na kuchukua chakula.
Akampeleka Salehe nyumbani kwake, baada ya kuhakikisha amejikomea mlango, akawasha gari hadi nyumbani kwa mpenzi wake.
“pole na mitihani mume wangu.” alipokelewa kwa sauti laini iliyomuondoa uchovu aliokua nao.
“Ahsante, hata hivyo mi sikai...” kabla hajaoendelea, mpenzi wake akabadilika sura na vitendo. Kutoka furaha hadi hali ya kususa.
“Nisikilize kwanza... Mi nilipanga nilale hapa usiku wa leo, ila kuna tukio kubwa limetokea na hivi sasa nahitajika niwe Muhimbili. Usichukie kipenzi, nikiwahi kutoka huko; nakuja huku moja kwa moja.” Inspekta Salim akabembeleza huku akiwa amemkumbatia mpenzi wake kwa nyuma.
“Naomba nikuambie kitu, kama kweli unataka niendelee kukufurahia.” Zamda aliongea hayo na kumgeukia mpenzi wake wakiwa katika hali ileile ya kukumbatiana.
“sema malaika wangu.” Inspekta akajibu huku akiachia tabasamu.
“hata ukirudi alfajiri, ila upitie hapa kwangu. Ulale mpaka muda wako wa kwenda kazini.” Zamda akaongea hayo huku uso wake ukiwa hauna hata chembe ya tabasamu.
“hilo tu, sema lengine laazizi.”
“na usipokuja?”
“Lazima nije mke wangu, labda yanikute mauti huko nji..” kabla hajamalizia, Shani akamziba mdomo.
“mara ngapi nimekuambia usinitajie maswala ya kifo. Darling nakupenda na sihitaji kukukosa.” Zamda akaongea kwa sauti ya kudeka huku akijilaza kifuani.
“nafahamu kama unanipenda, na dua zako zinaninusuru kila leo. Mimi naamini tutaishi muda mrefu hadi kuwaona vitukuu vyetu.”
Maneno hayo ya faraja yakaleta tabasamu kwa binti mrembo Zamda. Naye Inspekta akaaga kwa mara nyingine na kuruhusiwa kutoka.
Akafunga safari hadi hospitali ya Taifa Muhimbili. Ndipo alipompigia simu Samira ili ampatie maelekezo.
“siye tupo hapa kwenye mabenchi.. Tunasubiria tu maajabu ya Muumba katika kuyapigania maisha ya binti aliyeokoa maisha yangu.” Samira akajibu na kumfanya Inspekta Salim kusogea eneo hilo na kwenda kuegesha gari kwenye maegesho yaliyoruhusiwa.
Alifanikiwa kuonana na Samira akiwa na familia yake.
“Huyu ni baba yangu mzazi, anaitwa Mohammed; huyu ni dada yangu wa kuniachia ziwa... Anaitwa Rabia.” Samira alitambulisha na kumfanya Inspekta Salim ashikane nao mikono kwa mara nyingine.
“Baba, dada... Huyu ni Inspekta Salim. kwa kipindi hiki yupo karibu na mimi kwa haya majanga yote yanayoendelea kunikumba kila leo.” Samira aliongea hayo na kuwafanya watu hao watambuane kwa majina na vyeo vyao.
Yaliwachukua masaa mengine matatu kusubiri hapo, kabla jina la Samira kuitwa. Samira aliongozana na Inspekta Salim. Ila utaratibu wa kuingia mtu mmoja tu humo ndani, ulimfanya Inspekta Salim kutumia cheo chake na kuruhusiwa kuingia.
Waliweza kumuona yule kiumbe akipumulia mashine ya kumpatia hewa safi ya Oxygen. Walimtazama mgongoni ambapo alishafanyiwa upasuaji na muda huo alikua amebandikwa bandeji nyingi zilizoloa damu nyeusi.
Daktari aliwafuata na kuwapa pole.
“hali ya mgonjwa ni mbaya sana. Hata mapigo yake ya moyo hayadundi ipasavyo. Hivyo hapa tunajitahidi tu kuyapambania maisha yake kwa hizo mashine. Lakini hali si shwari.” Daktari aliongea hayo na kuwatazama Inspekta Salim na Samira.
Roho ya kike ikamtafuna Samira kwa kile alichokiona na kusikia kutoka kwa daktari, akajikuta akianza kulia palepale. Inspekta Salim alimtoa nje na kwenda kumkumbatia dada yake.
“vipi, huyo kiumbe amekufa?” Mohammed akauliza.
“hapana, ila hali yake ni mbaya sana. Sidhani kama atachukua hata masaa mawili.” Inspekta Salima akathibitisha hayo na kuwafanya waliopo nje kuingiwa na simanzi.
***********
Akiwa na ghadhabu, alitulia kwenye gari yake kwa muda kabla hajachukua uamuzi wa kuiwasha na kuondoka.
“Dokta Kelvin... Dokta Kelvin.” akaongea kwa sauti iliyojaa hasira huku akijiangalia kwenye kioo kidogo kilichopo mbele yake.
“Sauti ya kifo inaweza kukuita muda wowote.. Muda wowote ule kuanzia sasa.”
Dokta Miley akaongea hayo na kuwasha gari yake, akaitoa eneo hilo kwa kasi.
Akiwa njiani, simu ikaita, jina la Dokta Maliki likatokea kwenye kioo cha simu yake.
“Niambie ndugu yangu.” akaipokea kwa sauti iliyojaa upole, ila moyoni mwake akiwa na fukuto kubwa lililokua linamkereketa. Kutokea kwa Dokta Kelvin wakati akikaribia kutimiza azma yake, kulimfanya achafukwe nafsi yake.
“vipi, umefanikiwa?” Dokta Maliki akauliza swali lililomuongezea machungu, ghadhabu na fadhaa kwa wakati mmoja.
“kuna mshenzi amekuja kuleta taarifa ya msiba katikati ya shughuli..nadhani na yeye kifo chake kinapiga jaramba.” Dokta Miley akaongea huku akiwa makini na usukani. Maana mwendo aliokua akiendesha gari haukua rafiki kwa kufanya jambo lingine tofauti na uendeshaji.
“leo kweli tumefeli mazima.”
Kauli ya kukata tamaa, ndo iliyomfanya Dokta Miley aegeshe gari pembeni. Maana mshtuko wake ulitaka kumsababishia ajali mbaya kwa kugongana na roli lililokua limeomba njia kwa kumuwashia taa za hatari.
“wale washenzi wameshindwa kumuua Samira?” Dokta Miley akafoka.
“hata mimi nimekasirika balaa.. Mbaya zaidi risasi walizofyatua kwa ajili ya kumuua Samira, wamempiga mtu mwengine.”
Taarifa hizo zikawa za kuogepesha zaidi kwa Dokta Miley.
“naomba uniambie kuwa hawajakamatwa na wala hawajaonekana...” Dokta Miley akaongea huku moyo wake ukimdunda kwa hofu.
“hilo ndo la kushukuru.. Maana tulikua tunaukimbia mji sasa hivi. Maovu yote yangebumbuluka na mwisho wa siku tungefungwa miaka milioni 20 gerezani.” Dokta Maliki akaongea hayo na kumfanya Dokta Miley ashushe Pumzi.
“acha nifike kwanza hapo, kisha tutaongea vizuri. Maana naona kama hili dili linataka kututia mawenge.”
“Sawa.” Dakta Maliki akaongea hayo na kukata simu.
Kutokana na barabara kutokua na foleni nyakati hizo, Dokta Miley alitumia dakika ishirini tu kufika kwenye maficho yao.
“bado lisaa limoja tu tukaangalie michanganyiko yetu.” Dokta Maliki aliongea hayo baada ya kuangalia saa yake.
“nadhani italeta majibu mazuri. Hapa nawaza tu vile tutakavyoweza kuwa matajiri wakubwa hapa Afrika.” Dokta Miley akaongea maneno hayo na kumuangalia Dokta Maliki. Naye akaitikia kwa kutikisa kichwa.
Kusubiria dakika hamsini ili kutimia kile walichokihangia kwa muda mrefu, ilikua kama mwaka kwao. Walikaa, walilala, bado muda ulikua kama unasukumwa.
Hatimaye muda ukafika, mtambo maalumu waliotumia kuchanganyia michanganyiko yao ukafunguka.
Ulionekana uji mzito sana wa rangi ya kijani. Wote wawili wakaangaliana kisha wakatabasamu.
“haina haja ya kupoteza muda, tutafute mnyama wa kumjaribia.” Dokta Miley akaongea na kumtazama Dokta Maliki ambaye alionekana kuendelea kuchunguza mchanganyiko huo kwa kutumbukiza kifaa cha kupima joto.
“hatakiwi myama tu, bali mnyama jamii ya binaadamu. Aidha sokwe ama nyani.” Dokta Maliki akatoa kauli hiyo iliyofanya Dokta Miley akune kichwa.
“Sasa tutawapata wapi hao wanyama.... Na isitoshe hii michanganyiko hata hatujui inachukua muda gari kuishiwa nguvu kama haijahifadhiwa.” Dokta Miley akaongea huku akizunguka huku na huko.
“itachukua masaa sabini na mbili. Hivyo kama tukikosa hao wanyama, itabidi tumfanyie binaadamu majaribio.” Dokta Maliki akatoa wazo. Hapo ndipo Dokta Miley alipomuangalia na kuachia tabasamu.
Haya, michanganyiko imefanikiwa, ila wanahitaji majaribio ili kujua huo ugonjwa mpya unaleta madhara gani na watatumia dawa gani kuutibu. Je wataanza kuteka watu na kuanza kuwafanyia majaribio ili lengo lao litimie?
Vipi kuhusu kiumbe wa ajabu, hali yake ni mbaya na daktari amethibitisha kuwa hawezi kupona kutokana na damu zilizomtoka na kuathirika kwa mfumo wake wa upumuaji...
Tukutane tena Kesho iwapo tu nitapata share za kutosha, like kama zote na comment zenye kunionesha kama kweli mmesoma na mmeifurahia.
ukumbuke tu, hii ni TYPHIN, Hadithi ya kale inayoishi!
Muwe na usiku mwema.

TYPHIN 10

TYPHIN 10
‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
Aliangaza macho yake mlangoni ili kutazama kama kuna mtu anachungulia. Alipohakikisha kuna usalama wa kutosha, akauchukua mkono wa Mtafiti Gibson na kuanza kutafuta mshipa wa damu ili aweze kuipitisha sumu hiyo haraka kwenye mfumo wa damu.
Aliachia tabasabu baada ya kuupata, sasa alianza kulengesha sindano hiyo. Akachoma taratibu na kuhakikisha imefika mpaka mwisho.
“Kwa heri rafiki.” Dokta Gibsoni akaongea hayo na kuachia tabasamu.
Kabla hajabonyeza kitufe cha sindano hiyo ili kuruhusu bomba la sindano kupitisha sumu hiyo na kuingia kwenye mishipa ya damu, alishtushwa na sauti ikikohoa nyuma yake; alikua Dokta Kelvin.
“Dunia ni kubwa kuliko sisi... Hupaswi kufanya yote hayo kwa kushindana na dunia.” Dokta Kelvin aliongea hayo na kumfanya Dokta Miley aichomoe haraka sindano hiyo na kuitupia pembeni. Maana kichupa kilichuka kwenye kitoroli kidogo kiliweza kuonesha nembo ya sumu anayoitumia kwenye bomba hilo la sindano.
“kwa hiyo ulikua unanichunnguza?” Dokta Miley akauliza.
“hapana, nilisahau jambo muhimu sana, kumuachia nesi maagizo juu ya uangalizi unaotakikana kwa wagonjwa ambao wanaonekana wana ufahamu kwa macho, ila kiukweli hawana ufahamu. Ndo ikawa bahati kwake.” Dokta Kelvin akaongea hayo na kumfanya Dokta Miley amsogelee.
“mimi na wewe hatujaonana siku ya leo, hiki kilichotokea hujakishuhudia. Nitafurahi ukiacha kila ulichokiona kuwa siri yako.” Dokta Miley akaongea hayo na kuondoka kwenye chumba hicho bila kusubiri majibu yoyote kutoka kwa daktari mwenzake.
**********
Mlengaji alishahakikisha kwa kile alicholenga, akaachia risasi mbili haraka haraka zilizokwenda kwa spidi sana.
‘paaah, paah’
Milio ya kushtusha ilisika kwa sauti ndogo, ila urukaji wa damu iliyochafua shati la Mohammed, uliweza kuwafanya wapatwe na mshtuko.
Muanguko wa binti aliyepigwa risasi uliweza kuwajulisha baadhi ya watu waliokua hapo kwamba sehemu hiyo si salama.
Mlengaji akarudi garini haraka na kumuamuru dereva aondoe gari kwa kasi.
Kila mtu aljificha ili ajaribu kuokoa nafsi yake. Mohammed na binti yake Raniya walikua wamekumbatiana huku wakiwa hawaamini kilichotokea.
Simu ikaita kwenye gari alilokuwemo mlengaji.
“naam bosi.” mlengaji akaongea baada tu ya kupokea simu.
“bila shaka una habari njema za kunipa muda huu.” mkuu wa kitengo akauongea.
Mlengaji akatafakari kidogo, kisha akaongea.
“nilimuweka kabisa kwenye malengo, hata sijui kitu gani kimetokea. Nikajikuta nimempiga risasi mtu asiyehusika.” mlengaji akaongea hayo na kumfanya mkuu wa kitengo kupandwa na ghadhabu.
“unaniambia upuuzi gani? Kipi kilichokufanya umlenge mtu mwengine ilihali wewe ni hodari wa kazi yako?”
“wakati nalenga, huyo msichana hakuwepo... Ila baada ya kuachia risasi akawa amesimama mbele yake. Nikawa nimempiga yeye risasi zote mbili.” mlengaji akatoa ushuhuda.
“huyo msichana atakua hai kweli?” mkuu wa kitengo akauliza huku safari hii akiwa ameipooza sauti yake.
“sidhani kama atapona... Maana risasi zote zimepiga mgongoni.” Majibu hayo yakazidi kumnyong’onyesha.
“lakini una uhakika hakuna mtu aliyewaona?”
“ndio mkuu.”
Baada ya majibu hayo. Mtu aliyewapa kazi ya kumuua Samira akakata simu.
Dakika chache baadaye, askari walifika eneo hilo. Ni baada ya kupewa taarifa juu ya tukio lililotokea muda huo Triple Seven.
Watu walikua wamemzunguka binti aliyepigwa risasi na kuanguka chini. Kwakua alikua amedondokea kifudifudi, hakuna aliweza kuiona sura yake. Ila askari walipofika na kuugeuza mwili wa binti huyo, Samira alipigwa na butwaa baada ya kumuona binti yuleyule anayetangazwa kuleta madhara kila leo.
Alikua ananifuatilia, au nilitakiwa kuuwawa ndo ameniokoa? Samira alijiuliza swali hilo wakati walipokua kwenye kumbatio la baba yao aliyewasihi wabaki chini ya meza kwa usalama wao.
“baba, huyo binti aliyepigwa risasi. Ndo huyo aliyeniweka kisangani hadi nikaitwa polisi.” Samira alimuelezea baba yake, hapo ndipo naye akamtazama binti huyo kwa umakini.
Askari walikuja kuwatoa hapo walipo na kuwaambia kua wamezunguka maeneo yote na mahala hapo ni salama kwa muda huo. Waliwauliza kama kuna mtu amejeruhiwa baada ya nguo zao kuonekana kurukiwa na damu za binti huyo.
“Kwani amekufa?” Samira akauliza baada ya kuona wanamuingiza kwenye kwenye gari yao.
“hatujui, ndo tunamuwisha hospitali. Kwani unawafahamu ndugu zake?” Askari akauliza.
“Hapana, ila sura ya huyo binti si ngeni kwangu. Ningependa kujua anapelekwa hospitali gani.” Samira akauliza.
“Muhimbili.” Askari akajibu.
“tunawaze kuwafuatilia, nahitaji kujua maendeleao yake.... Hata kama kafa, nahitaji kujua pia.” Samira akaongea hayo na kumuangalia baba yake ambaye alikua anamminya kama ishara ya kumkataza kutojihusisha na maswala hayo.
“haina shida, tunaweza kuongozana.” Askari akajibu hivyo na kwenda kwenye gari iliyopandishwa mwili wa binti huyo, na yeye akaongozana na ndugu zake hadi kwenye gari yao.
“iwe kwa heri au ubaya, sijapenda kabisa maamuzi yako ya kushadadia watu. tena hawa askari, hawana muamana kabisa hasa kwa kesi kama hizi za mauaji. Wanaweza hata kusema wewe ndo shuhuda na uwasaidie kwenye upelelezi.” Mohammed alifoka walipokua njiani wakiifuatilia gari ya polisi.
“kuna uwezekano mkubwa zile risasi nilitakiwa kupigwa mimi... Maana usawa aliodondokea binti yule ni wangu kabisa. Kwanini tusihakikishe usalama wake? Na kama kafa kwanini tusiombe kuzika, maana nafahamu kama akili zake sio nzuri na hana ndugu wa kumfaa hata kwa nguo.” Samira aliongea maneno hayo na kumfanya baba yake awe mpole.
**********
Inspekta Salim akiwa hosptali, alifuata taratibu za awali na kumpeleka salehe kumuona daktari. Yeye alirudi kukaa benchi ili aweze kusubiri majibu ya vipimo atakavyopimwa mgonjwa wake.
Akiwa hapo, simu yake ikaita na jina la Samira ilikajitokeza.
“habari Samira, kwema?” Inspekta Salim alipokea simu hiyo huku akiwa na hofu, maana siku hiyo alihisi kujawa na mkosi.
“Mimi ni mzima kabisa. Ila kuna tukio limetoka Triple Seven muda mchache uliopita, yule kiumbe unayemtafuta; amepigwa risasi na watu wasiojulikana.” Samira akatanabaisha. Mapokeo ya mshangao yakazidi kwa Inspekta Salim.
“Amekufa?” akauliza kwa hamaki.
“kiukweli sijui, ndo tunamfuatilia hapa. Amechukuliwa na polisi anapelekwa Muhimbili muda huu.” Samira akamalizia kuelezea habari hiyo.
“mimi pia nipo hospitali, kuna kijana amevamiwa na watu haohao wasiojulikana. Ngoja nimalizane naye kisha nitawasiliana na wewe ili nijue mambo yanaendaje huko. Kwa lolote litakalotokea, usisite kuwasiliana na mimi.” Inspekta Salim akasisitiza.
“Sawa.” Samira akajibu na kukata simu. Akarejesha simu yake mkobani.
“hivi hakukutajia jina lake?” Mohammed akauliza baada ya kuona binti yake ameshamaliza kutoa taarifa kwa askari.
“sikumbuki chochote... Ila akifa roho itaniuma sana.” Samira akajibu na kumfanya Rabia amuangalie kwa jicho pembe.
“Usituchekeshe wakati tumetoka kunusika kufa... Yaani huyo binti anavyosababisha madhila kwa binaadamu bado unamuonea huruma? Na hao polisi hawajamjua tu, wangemmalizia kabisa kwa kumpiga risasi zingine.” Rabia akaongea, hata baba yake alimtazama.
“binti yangu, umeipata wapi roho ya kikatili kama hiyo?” Mohammed aliuliza na kumfanya Rabia aone aibu na kutazama chini.
Mwendo wa kuifuata barabara ukfikia kwenye kona, na baadae kwenye mzunguko na kuwajulisha kuwa wameshafika kwenye geti la kuingilia hospitali ya Muhimbili. Walichukua kadi ndogo kwa mlinzi na kuifuata gari ya polisi hadi sehemu ya wodi ya wagonjwa mahututi. Binti huyo akapokelewa, lilipohitajika jina moja kwa mtu aliye karibu naye, Samira alikubali liandikwe jina lake.
Watu wa huduma ya kwanza waliwahi na kitanda. Haraka akawahishwa wodini katika harakati za kuyapigania maisha yake.
Haya... Kiumbe wa ajabu yamemkuta. Alikua akijaribu kuokoa maisha ya Samira au na yeye alikua na dhamira nyingine? Endelea kufuatilia.
Ukumbuke tu....... Hii ni Typhin, Hadithi ya kale inayoishi...
Watu wengi hawana taarifa juu ya kurudi kwa riwaya hii ya kusisimua. Nisaidie ku-share ili iweze kuwafikia popote walipo. Ahsante!

TYPHIN 09

TYPHIN 09
‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
“sasa unasubiri nini kufanya kazi yako kama nafasi ipo?… muulie mbali.” Sauti ya mamlaka ikasikika upande wa pili, simu ikakatwa.
Taratibu kijana huyo alifungua begi lake na kutoa bunduki yenye uwezo wa kupiga masafa mrefu. Akafunga kiwambo cha sauti ili aweze kufanya tukio lake bila watu wengine kushtushwa na sauti ya risasi pindi atakapoifyatua.
Alihakikisha kama kuna risasi za kutosha, baadha ya kuridhika akaanza kuchungulia kwenye kifaa alichokifunga juu ya bastola hilo. Aliweza kumuweka Samira katika usawa mzuri. Alipandisha mshale wa malengo kwenye kifua cha binti huyo.
Samira akiwa anacheka, hakujua kua sekunde chache kutoka hapo hatokua hai endapo tu mlengaji atafyatua risasi kadhaa kifuani kwake.
Familia ilionekana kuwa na furaha sana kwa kutaniana na Samira hiki na kile. Mlengaji naye taratibu akapeleka kidole kwenye kifyatulio cha rasasi.
***********
Giza likiwa limetanda, hatua zikasikika zikisogea upande uliokua na mwanga wa taa. Akiwa peku, aliweza kufika eneo hilo lililokua na watu wawili wakipita na mmoja akifanya biashara. Alijisogeza hadi hapo kwenye biashara ya chipsi. Palikua na utulivu mkubwa kwakua hakukua na mtu mwingine zaidi ya muuzaji ambaye alikua anageuza chipsi zingine zilizokua jikoni. Alifika na kusimama hapo kwa muda bila kuongea kitu chochote, macho pima kwenye kabati lililosheheni vitu mbalimbali vya kutamanisha.
Muuza Chipsi alimshangaa binti huyo ambaye alisimama mbele ya kabati la chipsi bila kuongea kitu chochote.
“karibu dada, chipsi za moto zinatoka jikoni sasa hivi.” Muuza chipsi aliongea baada ya kuhisi huyo binti huenda ni mteja wake.
Hakujibiwa, zaidi binti huyo alikua akiwatumbulia macho samaki wakavu waliosimamishwa vizuri kwenye kabati hilo la chipsi.
“unahitaji samaki?” Muuza chipsi akauliza baada ya kutoka na kumsogelea binti huyo. Swali hilo likajibiwa kwa kichwa. Maana ni kweli alikua akihitaji.
“hawa wakubwa elfu tano na hawa wadogo elfu m bili mia tano.” muuza chipsi akanadi bei zake.
Binti huyo akaonesha samaki mkubwa aliyemvutia. Muuza chipsi akaenda kumchukua samaki hiyo na kumuweka kwenye mfumo.
“nikufungie pilipili?” muuza Chipsi akauliza, hakujibiwa.
Haikumshangaza sana, maana wasichana wengi wa mtaa huo walikua wakijisikia kutokana na maisha mazuri waliyoyakuta. Waliona hana hadhi ya kuwaongelesha zaidi ya kuwauzia wanachohitaji na yeye kupewa ujira wake.
Aliamua kumfungia binti huyo na kumletea. Alistaajabu baada ya kuona akifungua mfuko hapohapo na kuanza kumla bila kutoa miba. Baada ya kumaliza, alimuonesha samaki mwengine.
“hela ipo wapi kwanza.” muuza chipsi akauliza baada ya kumtazama binti huyo miguuni. Miguu ilikua imejaa vumbi; yupo peku, mwendo wa kumsaidia bata.
Kama mtu asiyeelewa lugha, binti huyo bado akakazania akaonesha samaki anayemuhitaji.
“we binti, utaenda kulala kwangu kama ukileta mchezo na pesa. Leta kwanza elfu kumi ndo nikupe samaki mwengine.” muuza chipsi akapandisha sauti.
Kwa kawaida binti huyo hua hapendi kelele, hasira zikaanza kumpanda kiasi cha kumuangalia muuza chipsi kwa macho makali.
Alipiga ngumi nzito kwenye kioo kilichopo mbele yake, kikavunjika. Akawatoa samaki wawili na kuanza kuwala kwa pupa huku akihema kwa kufoka kwa sauti ya kuogofya.
Muuza chipsi alishika kichwa kwa kile alichokiona muda huo. Wakati akiwa amepigwa na bumbuwazi asijue afanye nini kwa wakati huo, alimshuhudia binti huyo akifukutwa na kitu mfano wa moto kwenye koo lake. Hofu ya kuhisi binti huyo si binaadamu wa kawaida, ikamtanda.
Alipojaribu kukimbia, alipigwa ngwara na kuanguka kama gunia la viazi. Sasa mikono ikiwa juu akimuomba binti huyo asimdhuru. Maana tayari alishamfikia na kumzuia kwa kumkalia juu yake, uso wa binti alibadilika na kuwa wakutisha. Macho na shingo vilizidi kumtisha muuza chipsi kwa mngao wake mfano wa muwako wa moto.
************
“eeh Darling, upo wapi?”
“nipo njiani, naelekea kununua chipsi kwa Salehe.”
“Jamani, ujue Darling Chipsi si nzuri eeh, usiziendekeze sana.”
“Najua mume wangu, ila leo nimechoka sana. Acha tu nikanunue, kesho nitapika.”
“sikia, we rudi. Mimi naenda kununua samaki hapo kwa Salehe, mchele si upo?”
“ndio Darling.”
“basi we tulizana, miye mwenyewe nitaingia jikoni. See you soon.”
“ok, take care Darling.”
Hayo yalikua maongezi ya wapendanao. Inspekta Salim alikua njiani akielekea kwa mchumba wake. Hakujua kua wakati huo, Salehe muuza chipsi alikua katika hatua ngumu za kutetea maisha yake.
Baada ya kukata simu, alikanyaga mafuta ili kuwahi kwa Salehe. Alipaki gari yake na kushuka. Mshangao ukampata baada ya kuona mparakanyiko wa chipsi na vioo vilivyotapakaa kila mahali, alihisi kuna tatizo.
Akachomoa bastola yake ndogo aliyopenda kuiweka kwenye mfuko wa kote na kuanza kuangaza macho yake huku na huko.
Eneo hilo lilikua kimya sana. Na hiyo ni kutokana na kupooza kwa mtaa huo. Giza linapoingia, ndo kabisaa. Isingekua wateja kadhaa ambao hupata huduma mida ya usiku hasa hapo kwa Salehe, basi ungemshauri asifanye biashara usiku kwa usalama wake binafsi.
Inspekta Salehe aliita jina la muuza chipsi bila ya mafanikio. Aliingia kwenye fremu yake na kuangaza maeneo ya karibu, hakumuona pia.
“Haloo Darling, nahisi Salehe amevamiwa na watu wabaya. Acha nifuatilie. Nitakuja na chipsi tu. Ila uvumilie hata kama nikichelewa.” Inspekta Salim akapiga simu kwa mchumba wake na kumpa taarifa. Wakati akiwa makini huku bastola yake ameiweka vizuri, aliweza kusikia sauti kwa mbali ya mtu akihema. Aliwahi mtaroni ambapo ndipo sauti hiyo inapotoka, aliweza kumuona Salehe na kumsaidia kutoka.
Alikua anaweweseka huku moyo ukimdunda kupita kiasi.
“Tulia, upo kwenye mikono salama.” Inspekta Salim alimtuliza Salehe. Akamkokota hadi kwenye fremu yake ya biashara.
Hakutaka kumuuliza chochote kwa wakati huo zaidi ya kuanza kumkagua. Baada ya kuhakikisha amepumzika kwa muda wa dakika kumi, ndipo alipoanza kumuhoji.
“umeumia sana?” Inspekta salim aliuliza baada ya kutoona majera nje ya mwili wake.
“hapana.” Salehe akajibu.
“unaweza kunieleza ni kipi kilichokukumba?” Inspekta akauliza. Salehe akatingisha kichwa, akikanusha kuelezea.
Inspekta alitambua hali aliyokua nayo Salehe kwa muda huo.
“Tulia, acha nikusaidie kuweka vitu ndani. Tufunge na tuelekee hospitali.” Inspekta Salim akaongea hayo na kwenda nje. Akaanza kuingiza vitu ndani mpaka alipomaliza.
Baada ya kufunga, aliongozana na Salehe hadi kwenye gari yake. Akatekenya funguo na safari ya kuelekea hospitali ikaanzia hapo.
“nimefanikiwa kumpata, ndo tunaelekea hospitali muda huu.” Inspekta Salim alimpasha habari mchumba wake.
“Mungu mkubwa, kaumia sana?”
“Hana majeraha kwa nje… ila kwa hali yake, nahisi kaumia ndani kwa ndani. Ndo maana nampeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi.”
“sawa, utanijuza basi hali inavyoendelea.” mpenzi wa Inspekta Salim akaongea hayo na kukata simu.
**********
Baada ya kupatikana kwa utulivu wa hali ya juu, Dokta Miley alimuangalia Mtafiti Gibson kwa macho ya hasira.
“Natamani ungekua na kumbukumbu zako ili uweze kuniona kwanza muuaji wako siku ya leo. Ulikua unatamba sana kwa tafiti zako na ukatufanya sisi tunaokesha kufanya vitu bora zaidi yako tuonekane si lolote si chochote. Sasa leo ndo mwisho wako, na jina la Dokta Miley linaenda kufuta kumbukumbu zako zote. Ulikua rafiki hapo awali kabla hatujamaliza chuo, ila kwa sasa umekua adui wa jina langu. Ulale salama Gibson.”
Dokta Miley akachukua Sindano iliyokua kwenye mkoba wake na kichupa kidogo kilichokua na sumu ndani yake. Akavuta sumu hiyo iliyokua kwenye kichupa kwenye sindano tupu na kuhakikisha imejaa mpaka mwisho.
Aliangaza macho yake mlangoni ili kutazama kama kuna mtu anachungulia. Alipohakikisha kuna usalama wa kutosha, akauchukua mkono wa Mtafiti Gibson na kuanza kutafuta mshipa wa damu ili aweze kuipitisha sumu hiyo haraka kwenye mfumo wa damu.
Aliachia tabasabu baada ya kuupata, sasa alianza kulengesha sindano hiyo. Akachoma taratibu na kuhakikisha imefika mpaka mwisho.
“Kwa heri rafiki.” Dokta Gibsoni akaongea hayo na kuachia tabasamu.
Inaweza kuwa majonzi kwenye sehemu inayofuata. Tukutane tena Jumatano.
Kumbuka tu, hii ni TYPHIN, Hadithi ya kale inayoishi…
Kama umeipenda… like, comment kisha share na wenzako wapate kuifuatilia. Uwe na usiku mwema.

TYPHIN 08


TYPHIN 08
‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
“nitadili na Mtafiti Gibson, maana mimi ndo mwangalizi wake kule hospitali. Wewe andaa watu wa kuuondoa uhai wa Samira.” Dokta Miley akagawa majukumu na wote wakakubaliana nayo.
***********
Juhudi za madaktari wazoefu, pamoja na Kundra na Muumba ardhi na vilivyomo,zilionesha ahueni kwa mgonjwa aliyekaribia kupoteza maisha. Upasuaji mkubwa uliofanyika kwa kutoa miba ndani ya mwili pamoja na kuziba majeraha makubwa kwa kushona nyuzi nyingi, ndo yaliyoweza kumfanya mgonjwa huyo kuhamishwa chumba cha wagonjwa mahututi, hadi kwenye chumba maalumu ambacho waliandaliwa manesi wa kuhakikisha wanampatia mgonjwa mahitaji yote muhimu. Maana serikali ilikua inamtegemea sana mtu huyo katika tafiti za maswala ya baharini.
Akiwa chumbani, mgonjwa aliyekaribia kufa akapata ahueni, akafumbua macho. Tukio hilo lilimshtua nesi na kumfanya atoke mbio hadi kwenye chumba cha Daktari.
“Dokta, mgonjwa amefumbua macho.” Nesi akatoa maelezo yaliyofanya dakati huyo atabasamu na kunyanyuka kitini. Akamfuata nesi huyo mguu mosi, mguu pili hadi kwenye chumba cha mgonjwa.
“Sasa yale matumaini tuliyokua tunayasubiria, yameleta majibu mapema.” Daktri akaongea maneno hayo na kuchukua jukumu la kuanza kumpima vipimo mbalimbali.
Daktari aligundua kitu kingine, japokua Mtafiti Gibson alikua amefumbua macho, ila kumbukumbu zake bado hazijarejea.
“anahitaji uangalizi wa karibu sana. Mimi muda wangu wa kuwepo hapa hospitali umeisha. Dokta Miley akifika utampa hii karatasi ya vipimo nilivyompima. Yeye atajua kipi kitafuata baada ya hapa.” Daktari akatoa maelekezo kwa nesi huyo kisha akaondoka.
Nusu saa baadae, dokta Miley akafika hospitali na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha mgonjwa, alishtuka baada ya kumuona amefumbua macho.
“Hana kumbukumbu, Dokta Kelvin ameniachia hii karatasi ya baadhi ya vipimo alivyochukua. Amesema nikupatie.”
Dokta Miley akaichukua karatasi hiyo na kuanza kusoma baadhi ya mambo yaliyoandikwa.
“unaweza kuendelea na shughuli zingine… we niache tu na mgonjwa.” Dokta Miley akatoa kauli hiyo. Nesi bila kufahamu dhamira ya Dokta Miley, akatoka na kuwaacha watu hao wawili tu kwenye chumba hicho.
*************
Baada ya safari ya muda mfupi, Samira aliwasili nyumbani kwake. Bado alikua na hofu kubwa juu ya Watafiti wenzake. Alipitiliza chumbani kwake na kujilaza kitandani. Alianza kuchojoa nguo zake taratibu na kuelekea bafuni. Huko akajitumbukiza kwenye jakuzi. Alimaliza saa nzima huko akitafakari hiki na kile.
Alijitoa kwenye jakuzi taratibu na kwenda kitandani kwake akiwa utupu. Akachukua taulo na kujifuta maji, kisha akajifunga kifuani mwake.
Kila apatapo jambo zito, hupenda kuwasiliana na baba yake. Maana siku hiyo tayari Mzee Mohammed alikua Dar. Alichukua simu yake na kumpiga.
“niambie binti yangu mpendwa.” Mohammed aliongea baada ya salamu.
“baba, Watafiti wenzangu hawajaonekana mpaka leo hii. Hata simu zao hazipatikani. Kingine cha kutia wasiwasi, kuna watu wasiojulikana wamevamia maabara yetu.” Samira akatoa taarifa hizo kwa baba yake.
“Sasa umetoa taarifa polisi?”
“ndio baba, na Inspekta ameshauri tufunge Maabara kwa muda ili kupisha upelelezi, baba naanza kuogopa.” Samira akaongea na kumfanya Baba yake naye apatwe na hofu.
“ni nyema ukaenda kukaa kwa dada yako mpaka hili vuguvugu liishe. Binti yangu unakutana na visanga wiki hii, au kuna mtu umepishana naye kauli?”
“hapana baba, nahisi ni watu wabaya tu ambao hawapendi vile serikali inavyotuamini na kufanya kazi na sisi.” Maelezo ya Samira yakamfanya baba akusanye vitu vyake.
“upo nyumbani muda huu?” akauliza.
“Ndio baba.”
“jiandae, nakuja na Rabia hapo kwako kukuchukua.” Mohammed aliongea hayo na kukata simu.
“funga vitu vyako, mdogo wako yupo hatarini.. fanya hima tumfuate.” Mohammed aliongea maneno hayo na kumfanya Rabia ashangae.
“kakumbwa na balaa gani tena mdogo wangu?” Rabia akauliza huku na yeye akiweka vitu vyake kwenye mkoba.
“ni mambo ya kazini kwao, nadhani yeye mwenyewe atatueleza kinaga ubaga kuhusiana na hili.” akaongea na kumazama mtoto wake ambaye alikua anamalizia kuweka laptop yake kwenye mkoba. Akaongozana na binti yake hadi alipopaki gari yake, safari ya kwenda kwa Samira ikaanza.
Walipofika nyumbani kwa Samira, waliona kuna gari aina ya Noah nyeusi ikitoka eneo hilo. Iliwashangaza kidogo, maana nyumba anayoishi Samira ilikua ni ya mwisho kwenye mtaa huo. Hivyo gari yoyote iliyotoka hapo, ilimaanisha kua ilikua inatoka nyumbani kwa Samira.
“baba nina wasiwasi, huenda si watu wazuri hawa tuliopishana nao. Mbona walipotuona sisi tunakuja wamegeuza gari haraka?” Rabia akiongea maneno yaliyomtia hofu baba yake. Wakati huo walilishalifikia geti la nyumba ya Samira. Baba akachukua simu yake na kumpigia.
“Haloo baba.” Samira akaongea na kumfanya baba yake ashushe pumzi.
“wavaa mawe huko ndani… twende zetu. Muda si rafiki huu.” Mohammed aliongea hayo na kukata simu.
Samira alimalizia hereni zake na kuweka nguo kadhaa kwenye begi lake. Kisha akatoka na kumuachia mlinzi maagizo.
“huyo unayemuachia nyumba si mlinzi , nadhani unahitaji wale wenye bunduki, huyo mwenye kirungu hawezi kukusaidia ukivamiwa. Zaidi atakimbia tu na kukuachia dhahma.” Mohammed akaongea hayo na kuwafanya binti zake wacheke.
Mara zote Mohammed anakua baba bora kwa watoto wake. Huwezi jua kama ni baba na binti zake kwa jinsi walivyoshibana na kuwapa uhuru. Ilifikia hatua hata mama yao kutamani angejumuika nao kwa jinsi wanavyomtumia picha wakiwa sehemu mbalimbali walizopelekwa na baba yao.
Jioni hiyo aliwapeleka mahala tulivu ili wapate chakula cha usiku pamoja, kisha ndo awapeleke wakapumzike na yeye ndo arudi kwake.
Wakati wanafurahia chakula, hawakujua kama walikua wanafuatiliwa. Ile Noah nyeusi waliyopishana nayo awali, haikuwa ya heri kwa binti Mohammed. Kufika kwao ndo ilikua salama ya Samira, maana tayari vijana walishapewa kazi kwa ajili kuondoa uhai wake.
“bosi, tumefanikiwa kuwafuatilia hadi hapa Tripple Seven. hapa tulipo tunayo nafasi ya kumpiga risasi pia, au tuendelee kusubiri hadi atakaporudishwa?.” mmoja wa watu makatili, akatoa taarifa kwa mtu aliyempa kazi.
“sasa unasubiri nini kufanya kazi yako kama nafasi ipo?… muulie mbali.” Sauti ya mamlaka ikasikika upande wa pili, simu ikakatwa.
Taratibu kijana huyo alifungua begi lake na kutoa bunduki yenye uwezo wa kupiga masafa mrefu. Akafunga kiwambo cha sauti ili aweze kufanya tukio lake bila watu wengine kushtushwa na sauti ya risasi pindi atakapoifyatua..
Mimi na wewe hatujui nini kitakachomkumba binti Mohammed, vipi kuhusu uhai wa Mtafiti Gibson? Tukutane tena Jumatatu.
Simulizi hii itakua inaruka Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi.

DEREVA TOYO 12


Dereva toyo Mtunzi:Richard Yassin Sehemu ya 12 Bila kupata jawabu sahihi la kuhusiana na ni kwanini nilikuja na gari lile?Na ni sababu gani iliyonifanya nivae vile?Yote yalikuwa ni maswali ambayo niliyasikia wamama hao wakiyauliza pindi nilipokuwa chumbani kwangu. Mawazo yalinijaa nilipokuwa nafikiria ni kwa vipi nitumie zile pesa ili ziweze kuniletea pesa tele na kufanya niishi vizuri na nisitegemee tena kazi za kuajiriwa. Hivyo kutokana na kuwa na dimbwi la mawazo nilijikuta nimelala hadi ilipotimu mnamo majira ya saa 2 usiku muda ambao ulikuwa wa taarifa ya habari. Muda huo nilikaa kando ya televisheni ili niweze kujiona na ilipofika wasaa wa taarifa za kibiashara,taarifa yetu ilikuwa ya kwanza kuruka hewani.Ilikuwa ni mara ya kwanza katika maisha kujiona katika luninga.Na kwa bahati nzuri washindi wote tulionyeshwa tukipokea hundi hizo pamoja na kutoa machache yaliyoko moyoni kutokana na droo ambayo ilikuwa ikichezeshwa.Haikupita hata dakika 20 tangu habari ile ionekane nilipigiwa simu na Angel msichana ambaye tayari chem chem za mahaba zilianza kutiririka katika damu zetu ingawa alikuwa ameolewa. "Hongera darling kwa kujishindia.Naamini kwa sasa nyota yako ya mafanikio imeanza kuonekana.Na kwa kitita hiko ulichokipata naomba ukanunue toyo na nyingine weka benki kwani itakusaidia katika maisha ya mbeleni."Nilikaa kimya nikizidi kumsikiliza mrembo Angel akitoa nasaha zake kwangu.Siyo siri nilifarijika kutokana na ushauri alioutoa mrembo huyu.Na niliamini kwamba mrembo huyu aliletwa makusudi ili aniongoze katika nuru ya mafanikio ya ulimwengu huu na......Itaendelea!!!

DEREVA TOYO 11


Dereva toyo Mtunzi:Richard Yassin Sehemu ya 11 Kwangu suala hili lilikuwa gumu kwani kusimama mbele ya kamera na kutoa maneno ya kutia moyo kuhusiana na michezo ya kubahatisha ilikuwa ngumu ila nilijikaza kisabuni na kusema walau machache kuhusiana na michezo hiyo ya kubahatisha.Hivyo mara baada ya kila mshindi kuchukua hundi aliyojishindia,kampuni ilifadhili usafiri uliotupeleka hadi majumbani mwetu mara baada ya sherehe hiyo kumalizika.Nami kwa mara ya kwanza nilipata bahati ya kuingia katika gari aina ya Toyota Landcruiser Vx Model 2018 gari ambazo hutumiwa na viongozi wengi wa kiserikali. Ama kwa hakika nafsi yangu ilipata amani na furaha kwani sikuwahi fikiria kupanda gari kama hilo.Hivyo nilipiga picha na kuandika namba ya simu ili watulete picha hizo. Nilipofika nyumbani baadhi ya majirani waliokuwa wako nje hawakuamini kuona gari hilo likija maeneo yale.Nami bila kujali macho yao nilishuka kwa kujiamini kisha nikafunga mlango wa gari mara baada ya kumuaga dereva na kisha gari hilo liligeuza na kuondoka.Kitendo hiko kiliibua kicheko kikali kwani kama unavyojua asili ya uswahilini watu hawaachi umbea na kusema mambo yasiyowahusu.Hivyo ilinilazimu kuziba masikio na kuingia ndani huku nikiwaacha wamama hao waliokuwa wamekaa kibarazani kunijadili bila kupata jawabu sahihi la.....Itaendelea!!!

Friday, January 10, 2020

DEREVA TOYO 10


Dereva toyo Mtunzi:Richard Yassin Sehemu ya 10 Kwani katika dunia hii si rahisi kuamini mtu usiyemjua. Kwa hiyo kwangu mimi nilitamani muda ufike ili tupate wasaa wa kukabidhiwa kitita hiko. Watu walikaa kimya wakisubiria vigogo wa benk hiyo waingie.Hivyo tukiwa ndani ya benki hiyo tulihudumiwa kama wafalme kwani tuliletewa kikombe cha kahawa kila mmoja pamoja na half cake bila kusahau maji ya kopo.Kwangu mimi ilikuwa ni historia katika maisha yangu kwani sikuwahi kuhudumiwa hivyo kama mfalme na kuingia ndani ya ofisi yenye kiyoyozi.Nilitamani ningekuwa na simu janja nipige walau picha ya ukumbusho ila ndo sikuwa nayo. Muda ulifika wageni rasmi waliingia na wakiwa wameambatana na baadhi ya wafanyakazi wa NMB.Kitendo cha kuwaona wao kiliibua furaha kwa sisi washindi wa droo hiyo kwani tulipiga makofi kwa nguvu bila kuacha.Na hatimaye wageni hao waliketi nasi tukaketi pia.Punde zoezi la ugawaji wa zawadi hizo toka kwa washindi ukaanza.Nami jina langu lilitajwa.Nilinyanyuka na kwenda kupokea hundi ya mil.5.Kwangu mimi pesa hii sikuwahi ikamata tangu kuzaliwa kwangu.Na hii ilitokana na mizunguko yangu ya kifedha kutofikia kiwango kwani kwa kipindi hiko nilikuwa muajiriwa na mshahara wangu ulikuwa duni.Hivyo niliipokea hundi hiyo kwa furaha na kisha kabla sijaenda kuketi niliambiwa niseme jambo lolote kuhusiana na mchezo huu wa kubahatisha kwa watanzania.Kwangu suala hili lilikuwa gumu kwani....Itaendelea!!!

DEREVA TOYO 09


Dereva toyo Mtunzi:Richard Yassin Sehemu ya 9 Wasiojua maana ya usiri katika mioyo yao.Kwangu mimi niliandika historia kwani sikuwahi kupinduka na mama wa makamo na kumgalagaza.Hivyo kutokana na njaa niliamua kwenda kupata chakula cha kutuliza minyoo iliyokuwa ikinisumbua katika tumbo langu na nilipomaliza kula niliona ni vyema nirudi kupumzika.Nilingia ndani na kuweka muziki laini uliokuwa ukinibembeleza ila safari hii niliishia kulala na kutokana na uchovu nilijikuta kumepambazuka na sikuwa nimeweka neti.Asubuhi niliamka kama ilivyo ada nikanyoosha nguo zangu zilizokaa mkao mzuri wa kung'aa ili niweze kwenda kutunukiwa zawadi yangu.Nilivaa shati jeupe na suruali ya bluu huku nikitundika koti la bluu na tai ya bluu.Kwa namna nilivyovaa mtu wa kawaida angehisi kuwa ninafanya kazi ya uanasheria mjini.Hivyo nilipomaliza kuvaa moja kwa moja nilikwenda kuchukua uba ili inikimbize hadi maeneo ya Mlimani city mahala ambapo palifanyika makabidhiano ya pesa hizo katika moja wapo ya matawi ya benki ya Nmb.Siyo siri siku hiyo niliitendea heshima ya suti kwani waswahili husema unapovaa suti hairuhusiwi: 1. Kutembea kwa miguu masafa marefu. 2.Kula kwa kutumia kiganja. 3.Kujifuta jasho kwa mkono 4.Kula barabarani na mengine mengi. Hivyo mara tu nilipotoka nje ma Abasi alinotupia maneno yake ya kusifu maneno ambayo yaliukosha moyo wangu ingawa nilikuwa sina hela mfukoni kwangu kwani kwa sifa zile nilizopewa ningemtuza.Hivyo kutokana na kuwa na usafiri binafsi nilifika eneo la Mlimani City ndani ya muda mfupi.Na nilipofika nilionyesha kitambulisho changu ili watambue jina langu na hivyo walipoliona jina l hilo,nilikaribishwa na kukaa viti maalumu ili kusubiria uongozi mzima uje kuwakabidhi watu pesa zao walizojishindia.Nachoshukuru sikuwa peke yangu kwani palikuwa na watu wengine wawili waliojitwalia pesa hizo pia ingawa viwango vilikuwa tofauti na kila mmoja ilikuwa ni siri yake kwani....Itaendelea!!!

TYPHIN 07


TYPHIN 07
‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
“Nataka maji.”
kwa mara ya kwanza aliweza kuisikia sauti ya binti huyo mwenye macho makali ikimuamrisha. Akajikuta akikubali kwa kichwa huku sauti ikigoma kutoka. Akashtushwa na sauti za honi kutoka nyuma yake, maana muda huo taa zilisharuhusu na alikua amebung’aa tu baada ya kumuona binti huyo mwenye maajabu akiwa ndani ya gari yake.
Hakujua alipanda wakati gani, na amemfuata akiwa na nia gani baada ya kumfanyia vitimbi usiku wa siku iliyopita.
Akaondoa gari kwa spidi na kwenda kuiegesha kwenye kituo cha daladala ili aweze kumnunulia maji binti huyo. Akiwa na kitete, alimuita muuza maji na kununua maji yale makubwa kuliko yote kwenye deli lake la kuuzia. Akampatia binti huyo ambaye aliyapokea na kuyatupa nje kwa hasira.
Si inspekta Salim pekee aliyeshangazwa na kitendo hicho, bali hata muuza maji pia alikumbwa na hali hiyo. Ili yasitokee mengine ya kushangaza na kuwafahamisha watu wengine kua hakua na binaadamu wa kawaida ndani ya gari yake, aliamua kuondoa gari na kujaribu kumuhoji binti huyo alikua anahitaji maji ya aina gani.
Ububu ukatawala kwa kila swali alilomuuliza, binti huyo hakujibu kitu chochote zaidi ya kutazama nje na kuduwaa baada ya kuona mazingira yaliyompendeza machoni mwake.
Walipita maeneo ya daraja la Sarenda, ndipo binti huyo alipotabasamu baada ya kuona bahari.
“Simamisha gari.” Binti huyo akatoa amri nyingine, Inspekta Salim hakua na la ziada zaidi ya kuangalia usalama wa eneo hilo na kuegesha gari pembeni.
Kiumbe huyo akashuka na kuelekea upande uliokua na bahari. Hapo ndipo alipomshuhudia akikatisha barabara kila kuangalia magari.
“Kumbe alimaanisha anataka maji ya kuoga!” Inspekta alijisemea baada ya binti huyo kuelekea upande wa baharini. Alitamani kumfuatilia ili aweze kujua ni kipi kilichompelekea atamani kuoga muda huo, ila moyo wenye hofu ukamtuma aendelee na ratiba zake, maana binti huyo anaweza kumdhuru iwapo atagundua kua anamfuatilia. Alihisi kua binti huyo, inawezekana akawa hapendi kuangaliwa sana au kufuatiliwa ndo maana anaamua kuwadhuru wanaadamu au kushambulia magari pindi avukapo barabara.
“Nitaweza kumkamata huyu binti kweli?” Inspekta Salim akajiuliza huku akizidi kumtazama kiumbe huyo anavyoishia kwenye barabara.
Muda huohuo simu yake ikaita. Aliposoma jina, lilitokea la Samira. Akaipokea haraka.
“Inspekta Salim, kuna shida kidogo huku Maabara.” Samira akatanguliza kauli hiyo baada tu ya simu yake kupokelewa.
“kuna kitu gani tena kimetokea?” Inspekta Salim akauliza kwa hamaki.
“Kuna watu wamevamia maabara yetu na kuiba baadhi ya tafiti zetu. Kingine kinachonitia hofu, watafiti wenzangu simu zao bado hazipatikani.”
Taarifa ya Samira ilizidi kumfanya Inspekta Salim azidi kuchanganyikiwa.
“kwa sasa upo wapi?” Inspekta Salim akauliza.
“Nipo Maabara.”
“Nakuja.”
Inspekta Salim akaongea hayo na kukata simu. Hakutaka kumfuatilia tena binti huyo mwenye mauzauza. Lisaa limoja baadae, akafanikiwa kufika maabara na kumkuta Samira akiwa amekaa kinyonge. Muonekano wa maabara hiyo, ulionesha wazi kuvamiwa na kusachiwa.
Akapiga simu kituoni na kuomba msaada. Baada ya muda, walifika askari kadhaa na kuanza uchunguzi wa vitu mbalimbali.
“vipi kuhusu watafiti wenzako, unahisi wanaweza kuwa wamezama huko baharini?” Inspekta akamuuliza Samira baada ya kuhakikisha vitu muhimu vya uchunguzi vikiwa vimechukuliwa na wapelelezi.
“ndo hofu yangu kubwa… maana kulikua na taarifa za kuwepo na kiumbe wa ajabu baharini. Viumbe hao ndo wamewashambulia hawa samaki aina ya Golden, ni nadra sana kuwaona samaki hawa kwakua wanaishi kwenye maji ya kina kirefu na kupendelea kukaa sehemu zenye giza nene. Sasa kushambuliwa kwao ni wazi kuwa kuna viumbe hatari wamesogea baharini.” Samira akatoa maelezo hayo yaliyomfanya Inspekta Salim akune kichwa.
“itabidi niwashirikishe askari wa majini juu ya tukio hili… nadhani watafuatilia na kutupatia majibu sahihi juu ya hili jambo. Kwa sasa ningependa hii maabara ifungwe kwa muda ili kupisha huu upelelezi.” Inspekta Salim akaongea maneno hayo na Samira akakubaliana naye.
*************
Kwenye jengo la sukita, juu kabisa ya ghorofa, Dokta Miley akiwa na vijana wapatao nane waliojazia miili. Walikabidhi baadhi ya vitu kwake na yeye akawakabidhi pesa. Baada ya hapo kila mtu akiondoka kwa njia yake.
Akiwa kwenye gari, Dokta Miley akampigia simu mshirika wake.
“Dokta Maliki, vijana wamefanya kazi nzuri. Nadhani tunaweza kukutana muda huu ili nikukabidhi hii michanganyiko.” Dokta Miley aliongea maneno huyo huku akitabsamu. Akawasha gari yake na kuondoka eneo hilo baada ya kukubaliana ni wapi wawili hao watakutana.
Baada ya Mwendo wa masaa mawili, alifika eneo hilo na kukutana na Dokta Maliki.
“tumebakisha masaa kumi na mbili tu ili tuweze kupata michanganyiko mipya… na hizi tafiti tulizozipata, zinaweza kutusaidia kutengeneza vitu vingine vipya na kupata sifa kwenye serikali hii na Afrika kwa ujumla.” Dokta Maliki akaongea hayo na kumfanya Dokta Miley atafakari jambo.
“hizi tafiti kama zikifanikiwa kutuletea majibu maridhawa, basi inabidi kuna watu wapoteze maisha ili tubaki salama.” Dokta Miley akaongea maneno hayo na kumfanya Dokta Maliki ashtuke.
“wakina nani hao?”
“Mtafiti Gibson na msaidizi wake… maana hao ndo wanasauti kubwa sana serikalini. Wakisema kuwa sisi ndo tumechukua tafiti zao, wataaminika na sisi tutakua hatiani.” Dokta Miley akaongea hayo na kumfanya mwenzake atikise kichwa kama ishara ya kukubaliana naye.
“Mimi nitadili na Mtafiti Gibson, maana mimi ndo mwangalizi wake kule hospitali. Wewe andaa watu wa kuuondoa uhai wa Samira.” Dokta Miley akagawa majukumu na wote wakakubaliana nayo.
Haya, tamaa ya mali na kuwa na majina makubwa kupitia juhudi zilizofanywa na wenzao, zinawafanya Madaktari hawa kuingia katika dhamira ya kufanya mauaji baada ya kuiba tafiti ambazo wanaamini zitakua tiba kwa magonjwa sugu, hivyo zitawasaidia kutengeneza pesa nyingi.
Je Mtafiti Gibson na Samira watauwawa? Kipi kitakachotokea iwapo yatapita masaa 72 bila Inspekta Salim kumkamata kiumbe huyo aliyemshuhudia akielekea baharini?
Ukumbuke tu, hii ni Typhin… wingi wenu kwenye ufuatiliji ndo itakua inakuja mara nyingi kwa wiki.

TYPHIN 06


TYPHIN 06
‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
La haaulaaa!
Binti kapotea machoni mwake kwa kasi ya ajabu. Mbali na ujasiri mkubwa aliokuanao Inspekta Salim, kile kijasho chembamba cha woga kikaanza kumtiririka kwa kasi huku akikosa uamuzi wa kubaki kwenye gari ama kushuka ili amfuatilie binti huyo ni wapi alipoenda.
Akili ya ukombozi ikamwambia Inspekta Salim awashe gari yake na kuondoka eneo hilo haraka sana.
Kitete kikamfanya azime gari badala ya kuiruhusu iondoke. Akajikuta anahema mfano wa mtu aliyetoka kuogelea maji ya kina kirefu kushinda uwezo wake.
akazungusha funguo ya gari, safari hii gari nayo ikagoma kuwaka, akachachawa.
“waka baba, tutakufa hapa. Waka basi.” Akajikuta akilibembeleza gari huku akijaribu kuzungusha funguo mara kadhaa.
“Mbona betri bado jipya jamani… mbona linagoma kupiga stata?” akajiuliza mwenyewe huku akijaribu kuomba msaada kutoka kwa vitu visivyo na uhai. Uoga nao ukizidi kuutafuna moyo wake, harufu ya kifo alihisi inazidi kutanda ndani ya gari yake.
Alipojaribu kuiwasha gari hiyo kwa mara nyingine, safari hii ikakubali kuwaka.
Huo mwendo wake sasa, almanusura apate ajali kwa kuliingiza gari lake mtaroni kwa jinsi alivyokanyaga mafuta kwa nguvu.
Aliendesha gari yake kwa mfumo wa alijojo huku moyo wake ukidunda hobelahobela kwa hofu kuu aliyokuwa nayo wakati huo.
Alimshukuru Mungu na Malaika wake kwa kuweza kumfikisha salama usalimini nyumbani kwake na kuegesha gari nje ya geti. Alichokumbuka ni kuizima na kutoa funguo. Baada ya kufungua geti la nyumbani kwake, hakutamani kulirudia tena gari lake nje ili aliegeshe kwa usalama, aliona ni heri wezi wakaiba gari kuliko kutoka nje na kukutana tena na kiumbe huyo wa ajabu.
Aliingia ndani kwake na kujifungia, jasho lilitota kwenye nguo zake huku akihisi baridi mwilini mwake.
Aliliendea jokofu lake na kutoa kikontena kidogo kilichokua na mabarafu madogo madogo. Akachukua mzinga wa Joni Mtembezi na kuijaza kwenye bilauri iliyojaa barafu ndogo ndogo na kuanza kunywa kinywaji hicho kwa pupa.
“Hivi ni nimeonana na jini ama nipo kwenye ndoto?”
Inspekta Salim alijiuliza baada ya taswira ya binti huyo kujirudia kwenye ubongo wake. Kinywaji kiliendelea kushuka kwa fujo kwenye koo lake, lakini hakikuweza kumpa matokeao anayoyataka. Kimea kiligoma kabisa kuupumbaza ubongo wake.
Akajikusanya pale alipo na kwenda kujitupa kitandani kwake kama mzigo wa viazi. Akiwa hapo, alilazamisha usingizi, na baada ya muda ukakubali.
Alishtushwa na mlio wa simu yake, aliamka huku akiwa na wenge na kuangalia nani apigaye. Alipatwa na mshtuko mkubwa, akaipokea simu hiyo haraka.
“Mkuu!”
“hivi umesahau kama tuna miadi ya kukutana leo hii?”
“Nakuja mkuu, sasa hivi.”
Inspekta Salim akaongea maneno hayo, simu ikakatwa. Aliangalia saa yake ya ukutani, ilimsomea kuwa muda huo ni saa nne na nusu. Akajikusanya haraka hapo kitandani na kuelekea bafuni. Huko aliuchukua mswaki wake haraka na kuupeleka mdomoni bila kuweka dawa. Alifungulia maji kwenye bomba la mvua na kuanza kuoga huku akiendela kuswaki. Alifanya hayo yote ilimradi aweze kukimbizana na muda ambao mpaka wakati huo ulimshamtangulia.
Alitumia dakika kumi kujiandaa na kutoka. Akingia kwenye gari yake na kuelekea ofisini kwa mkuu wake wa idara.
Foleni nayo haikua rafiki mzuri kwake, aliishia kutukana madereva wenzake barabarani na kuna wakati alitamani hata kupanda juu ya magari mengine ilimradi awahi kufika ofisini kwa bosi wake.
Mpaka anaifika Posta, tayari ilishatimia saa tano na nusu. Alilaani kila kilichomchelewesha na kupiga hatua ndefu ndefu kuelekea kwenye lifti ili aweze kufika ghorofa ya saba.
Watumiaji nao wakawa wengi, hivyo lifti ikachelewa kushuka chini kwa dakika nne zaidi. Mpaka hapo, alikubali kuwa mpole. Ilipofika akaingia huku kichwa chake kikiwa na mawazo tele.
Baada ya kufika ghorofa ya saba, alisogea mapokezi na kuomba kuonana na mkuu wake. Akaruhusiwa baada ya dada wa mapokezi kufanya mawasiliano na kumtajia bosi wake ujio wa Inspekta Salim pale.
“Samahani Mkuu..” Inspekta Salim aliongea hayo alipofungua mlango, akaikatisha kauli yake baada ya kukuta kuna idadi ya watu wapatao wanne humo ndani.
“Karibu Inspekta Salim, tulikua tunakusubiri wewe tu hapa ili tuanze hiki kikao cha dharula.” Mkuu wa idara aliongea hayo na kumfanya Inspekta Salim aende kukaa kwenye moja ya viti vilivyopangwa vyema ofisini humo.
“Inspekta Salim, una haki ya kushangaa wingi wa watu tofauti na mategemeo ya miadi yetu. Ila kuna jambo limetokea na imetupasa tukutane kwakua wewe ndo unashikilia faili la kesi hiyo. Kuna binti analeta shida huko mitaani, umefikia wapi kwanza kwenye kutimiza majukumu yako juu ya hili jambo?”
Inspekta Salim alisisimkwa mwili baada ya kutajiwa habari za binti huyo.
“nalifanyia kazi mkuu, nipo kwenye hatua za mwishoni za kumtia nguvuni.” Inspekta Salim akajibu na kuwaangalia watu waliokua humo ndani kwa zamu.
“Inspekta Salim, hili jambo linaweza kukushushia heshima yako kama ukilichekea, hivi unafahamu hawa wanaokutazama ni kina nani?” swali hilo likamfanya Inspekta Salim awatazame tena watu hao ambao ni wageni machoni mwake.
“Hapana, bado sijawajua mkuu.” Inspekta Salim akajibu baada ya kujiridhisha kutowafahamu.
“Hawa ni wageni kutoka Rwanda, huyu ni Waziri wa mambo ya nje na hii ni familia yake. Leo hii asubuhi wameshambuliwa na huyo msichana na mtoto wao hivi sasa yupo hospitali. Sasa nakupa oda, baada ya masaa sabini na mbili, nataka nipate taarifa za kukamatwa kwa msichana huyo. Kama ni kichaa basi daktari athibitishe akiwa chini ya uangalizi wetu.” Mkuu wa kitengo akaongea maneno hayo na kumuangalia Inspekta Salim kwa macho makali.
“Sawa mkuu.”
ilikua ni Amri, hivyo kukubali ilikua ni lazima kwake. Akaruhusiwa aendelee na majukumu yake.
japokua alikubali kuifanya kazi hiyo, ila moyo wake ulitamani kusema jambo kwa mkuu wake juu ya kiumbe huyo ambaye ameyashuhudia kwa macho yake mauzauza aliyokuwa nayo.
baada ya kushoka kutoka kweli lifti, akaliendea gari lake taratibu tayari kwa kurudi kituoni ili aweze kupanga mikakati ya kumnasa kiumbe huyo.
“Kwanini anazuru watu?”
Inspekta Salim alijiuliza swali baada ya kufika kwenye foleni eneo la mataa.
Akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa, kioo kidogo kilichopo ndani ya gari yake, kilimuonesha kitu kilichomfanya ageuke nyuma haraka.
Hamadi!
uso wake ukakutana na sura ya binti huyo akiwa siti ya nyuma ya gari yake.
“Nataka maji.”
kwa mara ya kwanza aliweza kuisikia sauti ya binti huyo mwenye macho makali ikimuamrisha. Akajikuta akikubali kwa kichwa huku sauti ikigoma kutoka. Akashtushwa na sauti za honi kutoka nyuma yake, maana muda huo taa zilisharuhusu na alikua amebung’aa tu baada ya kumuona binti huyo mwenye maajabu akiwa ndani ya gari yake.
Hakujua alipanda wakati gani, na amemfuata akiwa na nia gani baada ya kumfanyia vitimbi usiku wa siku iliyopita.
Haya, waiteni ndugu zenu waje kwa wingi ili tuweze kuendelea…
Kumbuka tu, hii ni TYPHIN, Hadithi ya kale inayoishi………..

PAKUA APP YETU

Kwa wale wapenzi wa Mziki Mzuri,filamu nzuri na Hadithi nzuri kutoka kwa waandishi mbalimbali, blog yetu ya Burudani, Tunapenda Kuwataarifu kuwa:

> Kama Hautumii App Basi tunakuomba PAKUA APP YETU MPYA HAPA Ili uweze Kupakua Nyimbo Mpya kirahisi
> Pia Utapata Taarifa kila wimbo Mpya unapotufikia.

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Official android App for www.cleverwebtz.blogspot.com

This application is developed with the following key features:
• Listening Music online with latest collection of tracks
• Download Music for listening offline
• Read story from different author
•watch movies online and download
• Listen to Music and do other things with a convenient way with playing background modes, customizable through the Notification bar (notification).

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Last Updates

DEREVA TOYO 14