‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
Kiufupi ni binti wa kutolewa mfano pindi watu wakaapo kijiwe nongwa kusifia uumbaji wa Mola.
Hakika!
Wanaume hua tunasehemu zetu maalumu za kuangalia pindi tuyaelekezapo macho yetu kwa mabinti, ilichukua idadi ya wanaume kadhaa kutazama umbo la binti huyo kila akitzapo mahala. Ulimbo wa umbo lake, uliweza kuwafanya wanaume wakware kumtazama kuanzia utosini mpaka kwenye eneo la kiuno chake. Macho ya wengi yaliishia kutamtazama juu tu bila kung`amua kitu nadra kuonekana kwa binti mzuri kama huyo.
Licha ya kupendeza kwa baibui nadhifu, ushungi ulitupwa mabegani kiustadi baada ya kuzunguka kichwa na kuacha sura pekee ionekane. Hapo ndipo palipokua pumbazo kwa wanaume wengi pindi walipogandisha macho yao kwenye wajihi wa binti huyo. Licha ya weupe wake, upekee wa mboni zake uliwafanya wanaume wakware wazubae hata wasifahamu kua binti huyo alikua peku.
Naam!
Alikua akipekua mfano wa bata ama kuku atembeavyo, hakuonekana kujali tukio hilo la kustaajabisha kiasi hasa kwa binti mzuri kama yeye.
Kuinamisha kwake kichwa chini mfano wa binti mwenye aibu kila mara, hakukuweza kumtetea kwa udhaifu wake wa kutooona umuhimu wa viatu.
Nani angemsimamisha na kumuuliza kwanini alikua akipekua?
swali lilibaki uvunguni mwa moyo kwa waliomtaza. Ilikuwaje akakosa viatu ilihali baibui alilovaa ni la gharama sana? Kama aliacha viatu kwa fundi, ilikuwaje hata hajaomba viatu vya ziada au kusuiri mpaka viatu vyake vifanyiwe ukarabati?
Kila aliyegundua hali ya msichana huyo miguuni, alimeza tu fundo la mate kulibakisha swali lake ndani huku macho yakiendelea kupata ladha ya tukio hilo geni kutokea hasa kwa wasichana mrembo.
“Mambo dada.” Sauti iiyosikika vyema kwenye ngoma za masikio ya binti huyo, ilimfanya amuangalie kwa muda bila kumjibu kitu chochote.
“kama una tatizo niambie, naweza kukusaidia.” Kijana huyo akaongea tena na kujilazimisha kutabasamu.
Binti huyo hakujibu kitu chochote, alinyanyuka na kuanza kuvuka barabara.
Kiichomshangaza , ni vile msichana huyo hakua anajali magari wala kuangalia yanapotokea.
Kuna gari ilifika na kumpigia breki miguuni. Ilimgusa kidogo kutokana na mwendo kasi wa chombo hicho cha moto.
Mshangao!
binti hyo hakuanguka chini wala kutikisika.
Ilikua ni ajabu na kweli kwa kile walichokua wanakishuhudia muda huo. Binti huo akawaangalia tu na kuendelea na safari yake.
Dereva akashuka na kutazama gari yake, wakati huo yue kijana wa awali naye alikua ameungana na wahanga hao katika kutazama gari hiyo.
Laa haulaa!
Kuanzia ngao mpaka bodi ya gari, vyote vilikua vimebonyea. Mshangao mkubwa ukawapata na kuwafanya wasiamini macho yako kwa muda.
“yule msichana si binaadamu, yaani utafikiri tumegongana na gari?” dereva alipaza sauti baada ya kuona maajabu mapya ya dunia. Jambo lililomfanya mpaka mke wake apigwe na bimbuwazi.
“amefanyaje kwani?” mke wake akauliza huku akishuka kutoka kwenye gari. Kibegi chake mfano wa kipima joto kikiwa kwapani na kuungana na mume wake kwenye mashangao huo.
“Tupige simu polisi, hili tukio hakuna ambaye ataweza kuamini kama hajalishuhudia kwa macho yake.” mwanamke huyo akaongea huku akitoa simu kwenye pochi hiyo na kuanza kupiga picha eneo la gari lililopata athari.
*************
Ishara ya Baruti nyekundu iliyoonekana kwa mbali, iliweza kuwafahamisha askari maji kuwa kuna tatizo eneo fulani, hivyo boti za askari hao wa majini zilifika eneo husika.
Kwa msaada wa Helkopta, walifanikiwa kukiona chombo cha Mtafiti wa wanyama wa baharini, Mr. Gibson kikiwa kinaanza kuzama baada ya maji kuingia ndani na kukishinda uwezo wakuhimili.
Juhudi za kukizuia chombo hicho kisizame, zilifanyika kwa umakini mkubwa. Maana moja ya meli zilizofika eneo hilo, ilikua na uwezo mkubwa wa kuvuta vitu vizito. Hivyo waliwahi kuifunga minyororo na kufanikiwa kuipandisha juu kwa mara nyingine.
“Msaa…”
Ikasikika sauti ya mtu; sauti ambayo haikumalizia ni kipi alichohitaji kusema.
Sauti iiyosikika mita kadhaa kutoka walipo. Wataalamu hao wa kuyakata maji, wakazamia na kuelekea huko walipoisikia sauti hiyo.
Waliweza kumuona Mtafiti Gibson akiwa ameanza kuruhusu maji kuingia kinywani huku akitapatapa. Mtungi wa gesi aliouvaa haukuwepo tena mgongoni, Hakuweza kuendelea kuhimili, akapoteza fahamu kaba ya msaada kumfikia.
Taa zilizopo kwenye boti hiyo, ziliweza kuwaonesha majeraha makubwa aliyoyapata mtafiti huyo. Mbali na kutokua na fahamu, ila mwili waake ulionekana kujaa majeraha makubwa kupita kiasi.
“Tunaomba msaada wa Helkopta haraka iwezekanavyo ili kumuwahisha mgonjwa hospitalini. Hali yake ni mbaya sana.” Askari mmoja akafanya mawasiliano.
Helkopta iliyofanikia kuiona boti hiyo, ikafika na kumchukua mgonjwa haraka ili kuwahi kuokoa maisha yake.
Mbali na kuyapigania maisha yake alipokua kwenye maji kiasi cha kupoteza fahamu, ila mkono wake wa kushoto ulionekana umekunja ngumi kama ishara ya kung’ang’ania kitu fulani. Waliufungua, ndipo walipoweza kuona kifaa kidogo kilichokua na ncha mfano wa sindano. Huku ndani yake kukiwa na kimiminika ambacho hawakueza kukifahamu ni kipimo cha kitu gani.
“huenda ni tafiti zake muhimu alizofanikiwa kuzipata baada ya kuhatarisha maisha yake. Jitahidi kumtunzia.” mmoja wa askari aliyekua kwenye helkopta, alitoa wazo baada ya kuchukua kichupa hicho.
Hakuna aliyefahamu kipi kilichomsibu pindi alipokua baharini. Ila majeraha yaliyokua mwillini mwake yaliweza kuwafanya wahisi alishambuliwa na papa mkubwa pindi alipokua kwenye tafiti zake.
*******
SIKU MOJA KABLA:
Bado haitoshi, aliendelea kurudia kuwika mara kadhaa kama vile aliajiriwa au alfajiri iliumbwa kwa ajili yake ili awike. Tena karibu na dirisha la mtu asiyemfuga wala kumpa chakula pindi awapo na njaa.
Majira yakasadifu ukweli wa muonekano wa anga, Ilikua saa kumi na moja na nusu.
Licha ya chumba chake kuwa na kiwambo cha upepo baridi, feni la kawaida pia lilikuwepo. Lakini Samira alipenda kupata upepo mwanana wa angani hasa nyakati za usiku mkubwa. Hivyo hufungua dirisha la kioo na kuacha wavu uliosukwa kiustadi kupenyeza upepo mwanana wa anga la Muumba wetu.
Alifahamu kero hiyo ingekoma iwapo tu angefunga dirisha, maana lilikua na uzito ambao sauti ya jogoo isingeweza kupita kwa ukali kiasi hicho.
Akafunga huku akilaani sauti ya jogoo huyo aliyeukatisha usningizi mnono wenye ndoto za kupambaza akili.
Akarudia kujifunika shuka. Wapi! Usingizi ulishaenda zake.
Ilimchukua dakika kumi na tano kujigeuza kitandani bila kupata mrejesho wa maombi yake ya usingizi kwa awamu nyingine.
Akanyanyuka kwa hasira na kuelekea jikoni. Alipasha mikate kwenye kipashio cha umeme na kukaanga mayai matatu. Akachukua maziwa kwenye friji na kuyapasha kwenye birika dogo ya umeme.
Kwa kawaida Samira hupenda kupata kifungua kinywa cha vipande viwili vya mkate na mayai huku akishushia na maziwa kila aamkapo.
Maana huamini ndo humuondoa uvivu wa kwenda kazini kutokana na shughuli za kuandaa chakula hicho cha asubuhi.
Mara zote huandaa vitu hivyo akiwa na nguo ya ndani pekee. Maziwa yake madogo yalimfanya avae sidiria kama ushahidi tu ama urembo. Ila kwa stamala yake, yanaweza kusimama yenyewe tu.
Baada ya kupata kifungua kinywa ambacho hakikua kwenye ratiba ya siku hiyo, akaenda tena chumbani na kuelekea bafuni. Huko aliwasha kifaa cha kupasha maji moto kwenye jakuzi kisha na yeye kujitumbukiza ndani yake baada ya maji kufikia joto alilolihitaji.
Aliwasha radio yake iliyokua na flash, humo alipanga nyimbo kadhaa ambazo hupenda kuzisikiliza na kuzifuatisha awapo bafuni. Akapata burudani ya miziki huku akicheza na mapovu mengi aliyayotengeneza kwa machanganyiko wa sabuni mbalimbali za kunukia.
Baada ya kuitumia nguo yake ya ndani kama sumba la kuondolea uchafu mwilini mwake, aliifikicha na kuianika.
Akaliendea taulo na kujifuta vizuri huku akijichungulia kwenye kioo kama ana ugeni vile na maungo ya mwili wake.
Alijibenua kidogo ili aangalie uumbaji wa mola upande wake wa mgongoni, akatabasamu baada ya kuona mlima mdogo ambao ulimsaidia kumtofautisha na mwanaume.
Akatabasamu na kutoka chumbani.
“Niende maabara kweli? Ama nibaki tu nyumbani?” alijiuliza baada ya kufungua tu kabati la nguo zake.
Wakati anajishauri, kengele ya malango wake ikaita kwa ghadhabu. Akaghairisha zoezi la kutafuta nguo, akaamua kuliokota taulo lake kwa mara nyingine na kupiga hatua kadhaa kuuelekea mlango.
Alipofungua mlango wa kutokea barazani, alikutana an sura ya mlinzi wa nyumba hiyo.
“Kuna askari wapo nje, wamesema wanashida na wewe.”
Kauli hiyo ilimshtua sana Samira. Akaamua kutoka hivyo alivyo mpaka nje.
Kweli, alikutana na Gari ndogo ya askari huku wanaume wawili wamakamo waliova sare, wakiwa mlangoni.
“Bila shaka wewe ndo Samira Mohammed!” Askari mmoja wapo akauliza.
Huku moyo ukimdunda, alikubali.
“Kajiandae uongozane na sisi kituoni.”
Askari mwengine akatoa kauli hiyo. Sura zao zilionesha kuwa na ghadhabu kiasi cha kumnyima uhuru hata wa kuuliza kosa lake. Akakubali kwa kichwa na kuingia ndani.
Mwili mzima ulimtetema, hata yale madaha yake ya utembeaji yakapotea. Nusura taulo limdondoke na kumpa burudani ya macho mlinzi aliyekua akimshuhudia akiwa anatembea kama anasukumwa. Hakika tukio la kufuatwa na polisi mpaka nyumbani lilikua geni kwake. Aliwazoe wale wa usalama barabarani,ila sio hao waliokua na bunduki mikononi.
Amefanya nini tena huyu mrembo, vipi kuhusiana na kiumbe wa mwanzo,mtembea peku? Mtafiti atapona? Yapi aliyomsibu baharini?
Unaweza kuifuatilia riwaya hii kwa mfumo wa sauti murua ya Molito huko Youtube kwa ku search akaunti yake, Molito Brand.
Au kwa kubonyeza link a blue hapo chini
https://www.youtube.com/watch?v=HWk1-Bltj4U
Karibuni!








0 comments:
Post a Comment
comment