Hadithi za kuchekesha katika Afrika
Ninaweza kuanza na hadithi moja katika Zimbabwe. Nilienda Zimbabwe kabla ya uchaguzi na niliendesha kati ya Harare na Bulawayo (mji kubwa wa MDC). Kama kawaida pale Afrika, kuna polisi nyingi kando ya barabara na wanazuia kila gari wakati wanafikiri wanaweza kupata pesa au kupata vitu vya upinzani yao. Kwa kivyo nilizuiwa kila wakati niliona polisi kwa sababu mimi si mwafrika na wanajua labda nina pesa na nitalipa. Polisi moja, baada ya kujizuia barabarani, alisema nilihitaji kuwa na leseni ya Zimbabwe kuendesha na itakuwa ada kubwa. Nilisema leseni yangu ilikuwa ya kutosha kuendesha pale na sikuenda kulipa. Halafu alianza kutafuta gari langu wakati nilichungwa na polisi mwengine. Halafu kiongozi cha polisi ambaye alikuwa na bundee kubwa alijaa na alijiona na aliguta, "Wewe ni Peter Crouch!" Nilisema tu, "Mimi si Peter Crouch, jina langu ni Marcus" na alisema "Hapana najua wewe ni Peter Crouch, hamna shida, unaweza kuendelea." Halafu polisi yao walisimama kutafuto na niliondoka bila kulipa.
Baada ya kuondoka Zimbabwe nilijifunza Peter Crouch ni mchezaji maalum wa soka katika Uingereza, na alifanana mimi (labda). Kwa hivyo kiongozi cha polisi alifikiri mimi nilikuwa mchezaji wa soka. Tangu Zimbabwe nimevurugwa na Peter Crouch katika Afrika mara tatu tofauti na kila mara mtu anajiomba kusaini vitu vyao.








0 comments:
Post a Comment
comment