CLEVER WEB TZ

Breaking News
Loading…

Pages

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
ENEZA BIASHARA YAKO

Wednesday, December 11, 2019

DEREVA TOYO 01




Dereva toyo Mtunzi:Richard Yassin Contact:0714137918 Sehemu ya 1 Kijiji kizima kilizizima mara baada ya kushinda mimi jackpot kubwa iliyokuwa ikichezeshwa na kampuni moja maarufu ya michezo ya kubahatisha ya jijini Dar es Salaam.Nilipigiwa simu usiku na nikaweka loud speaker ili kila mtu asikie na punde si punde taarifa zilizagaa katika kijiji chote kuwa nimekuwa milionea hivyo kelele za furaha zilitapakaa kijiji chote.Na mi kutokana na ushindi huo wa takribani mil.5 nilishukuru maulana kwani kwa muda mrefu nilikuwa sina kazi mara baada ya kupunguzwa kazi katika shule moja maarufu ya kanisa iliyopo wilaya ya Same.Ila mara tu baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi walau miale ya mafanikio iliangaza tena katika maisha na kujiona kuwa ni mtu katika watu. Siku hiyo sikulala kwani mawazo ya kuwa na hela nyingi ilitawala usiku mzima.Hivyo niliweza kuisindikiza usiku kwa kuwa macho hadi asubuhi ilipopambazuka. Na palipokucha nilikwenda moja kwa moja hadi stendi ya Makanya nikitokea Tae mahala ambapo palikuwa ni kitovu kikuu cha safari ya kwenda mikoa jirani pamoja na nchi za nje.Hivyo nilipofika Makanya,nilipanda basi na taratibu safari ya kwenda katika jiji la Dar es Salaam ilianza. Njia nzima nilionekana ni mtu mwenye furaha tofauti na abiria wengine.Wengi wao walijawa na mashaka wengine walikuwa wamechoka hivyo nyuso zao zilijawa na hali ya kutochangamka. Tulipofika maeneo ya Hedaru alipanda mdada mmoja ambaye alikuja moja kwa moja hadi katika siti yangu.Nilifurahi sana kupata mrembo katika siti hiyo kwani nilijua kuwa watu wengi ni lazima watakuwa wanamtazama sana.Siyo siri mdada huyu aliumbika maana alikuwa na kichuguu mgongoni mwake,kifua saa sita na weupe. Hivyo uzuri wake ulimfanya awe kivutio cha utalii katika basi tangu alipoingia garini.Siyo siri hata mimi mapigo ya moyo yalirindima kutokana na uzuri wake. Hivyo nilipo ona amekwisha tulia barabara nami nilianza kuchanga karata zangu ili niweze ku....Itaendelea!!!

5 comments:

comment

PAKUA APP YETU

Kwa wale wapenzi wa Mziki Mzuri,filamu nzuri na Hadithi nzuri kutoka kwa waandishi mbalimbali, blog yetu ya Burudani, Tunapenda Kuwataarifu kuwa:

> Kama Hautumii App Basi tunakuomba PAKUA APP YETU MPYA HAPA Ili uweze Kupakua Nyimbo Mpya kirahisi
> Pia Utapata Taarifa kila wimbo Mpya unapotufikia.

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Official android App for www.cleverwebtz.blogspot.com

This application is developed with the following key features:
• Listening Music online with latest collection of tracks
• Download Music for listening offline
• Read story from different author
•watch movies online and download
• Listen to Music and do other things with a convenient way with playing background modes, customizable through the Notification bar (notification).

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Last Updates

DEREVA TOYO 14