Stori: Shabaha moja (Ukatili usio sahaulika)
Mtunzi: ABiClever Junior
Sehemu: 04
Tulipoishia>>Jesi akasema "sawa" kisha akaelekea kwenye ngazi ndogo ya kuingia ndani na akakaa kwenye ngazi hiyo na kushika kichwa huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
Inaendelea>> Gari ya wagonjwa iliyokuwa imebeba askari wawili waliofariki na mmoja aliyejeruhiwa iliwasili hospital haraka maiti zilipokelewa na wahusika na aliyejeruhiwa pia alipokelewa na wahusika.
*****TUKIRUDI UPANDE WA RAMSO*************
Ramso alichukuliwa na kupakizwa kwenye Gari ya wagonjwa na haraka kuwahishwa hospitali.
"aisee yule ni afande Ramso au ni macho yangu?"kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Stanley alikuwa akimuuliza Rafiki yake Jacob aliyekuwa naye pembeni kidogo na Tukio.
"Ndio mwenyewe yule mwana"alijibu Jacob kwa tabasamu la juu zaidi,
"hahahaha jamaa leo kapatikana"aliongea Stanley kwa kicheko.
***********HOSPITALI***************
"afande Benson inabidi wewe ubaki hapa na uwe mwangalifu kumuangalia afande Nikolas maana afande Ramso alinipigia simu na kuniambia kuwa ameona pikipiki tatu zikiwa zinatufatilia"aliongea mkuu wa kituo anachofanya kazi Ramso kumwambia afande benson.
"sawa mkubwa"alijibu afande benson kwa Heshma.
Mkubwa wa kituo(Samson)anachofanya kazi Ramso alitoka nje ya hospitali na muda si mrefu dereva wake alikuja kumchua na Gari aina ya Land Rover aliingia ndani ya Gari na kuondoka.
Wafuasi wa MonNyeusi hawakuwa mbali moja kwa moja na wao waliingia ndani ya Hospitali hiyo na kuanza kumsaka sebastian wakiwa na uhakika sebestian nayeye atakuwa kwenye Hospital hiyo.
"oya mnamuona yule askari pale mlangoni?"aliongea madkick kuwauliza wenzake.
"ndio tunamuona"walijibu kwa pamoja madboy na madlion.
"inabidi tumtaitishe yule askari ili atuambie sebastian yuko wapi?"aliongea madkick.
"sawa"wenzake walijibu.
Wakati wanataka kumfuata yule askari walisikia vishindo vya watu wanakuja mkukumkuku ikabidi wageukie ukutani ili kujificha.
Hapo alipitishwa Ramso kwa speed ili kwenda kufanyiwa matibabu.
"huyu ndio yule askar tulie mpiga risasi au siye?"aliuliza madboy.
"acha maswali Tufanye kilichotuleta"aliongea madkick.
Waliamua kujifanya kama wanaondoka kisha wakapita karibu na afande Benson na kumuekea bunduki ya tumbo "tulia kama ulivyo shida yetu sisi ni kujua wapi alipo sebastian"aliongea madlion kumsihi afande benson.
"kusema kweli hiyo ni siri ata mimi sikuambiwa alipopelekwa sebastian.
******NYUMBANI KWA MKUBWA WA KITUO********
"mke wangu usiku kucha sikulala kwa ajili ya tukio la jana"aliongea samson(mkuu wa Kituo)
"pole mume wangu"mke wa samson anayeitwa sara alimjibu mumewe.
Ghafla simu ya samson ikaita "haloo"samson aliongea baada ya kupokea.
"afande Ramso hali yake sio nzuri ameletwa sasa hivi hapa hospital inaoneka ameshambuliwa Risasi nyingi sana"aliongea Dokta Smith kumjulisha Samson kuhusu kilichomkuta Ramso.
********NYUMBANI KWA RAMSO************
Jesi aliamua kumtwangia simu Ramso.
"pokea basi simu ramso pokea pliiz"aliongea maneno hayo baada ya kuona simu aliyopiga haipokelewi.
***************HOSPITALI***********************
Dokta mmoja ambaye alikuwa na simu ya Ramso alipokea "haloo"
Jesi: samahani nataka kuongea na Ramso
dokta:wewe ni Nani yake
Jesi: mimi ni mdogo wake
Dokta: sawa ila Ramso hali yake mbaya na sasa yupo chumba cha Operesheni.
"acha kututania nadhani hutufahamu vizuri" aliongea mad lion kumtisha Benson huku akindingisha pua moja.
Madkick aliweka silencer kwenye bunduki yake na kupiga moja kwenye mguu wa Benson.
"hasssh hashh"
Hapo benson hakuwa na ubishi aliwaelekeza alipo sebastian.
Madkick hakupoteza muda akamuua kabisa Benson na kisha wakaondoka.
******NYUMBANI KWA RAMSO**************
Jesi alipoteza fahamu Baada ya taarifa alizozipata...
Itaendelea....................
0 comments:
Post a Comment
comment