inaendelea>> mnamo majira ya saa 8 usiku, ^trrrrr trrrr trrrr^ simu ya Ramso ilikuwa ikiita , kiuvivu kabisa Ramso alisogeza mkono wake wa kulia mpaka sehemu ilipo simu yake kisha akainyanyua na kutumia mkono wake wa kushoto kufikicha macho ili aweze kuona ni nani anapiga muda huo ,ilikuwa ni simu ya Ofisi haraka alipokea simu na kutega sikio.
"Ramso Tafadhali nakuomba ufike ofisini muda huu Kuna jambo Baya limetokea hapa ofisini" aliongea Mkuu wa Kituo anachofanya kazi Ramso.
"sawa Mkubwa"alijibu Ramso kisha haraka haraka alinyanyuka kitandani na Kuvaa suruali chapchap kisha akavuta flana iliyokuwa imetundikwa mlangoni" na haraka akafungua mlango wa chumbani kwake na kumuita jesi, Wakati huo jesi alikuwa amelala chumbani kwake.
"Jesi natoka njoo ufunge huu mlango wa Nje" aliongea Ramso Hakupoteza muda hakuweza hata kumsubir Jesi atoke chumbani.
Kisha alichukua pikipiki yake na kuipiga moto
"wewe Garasa amka mimi natoka fungua Geti hilo" maneno hayo aliongea Ramso kumtaka mfanyakazi wa Getini mwa Nyumba yake(Mlinzi) Afungue geti.
Baada ya saa Kadhaa aliwasili Kituoni, alishuka kwenye pikipiki yake.
alipigwa na Butwaa baada ya kukuta gari ya wagonjwa,gari za askari na askari wengi zaidi kituoni Hapo. Kwa mbali alimuona mkubwa wake, moja kwa moja alienda kwa mkubwa wake.
Ramso alitoa heshima kwa mkubwa wake kisha akauliza"Nini kimetokea hapa mkubwa?".
"ingia ndani ya kituo utajua nini kimetokea " alijibiwa na Mkubwa wake.
Ramso Bila ya kupoteza muda aliamua kuingia ndani ya Kituo.
********UPANDE WA WAMAGAIDI*************
"ni uzembe imekuaje mpaka mmemuacha sebastian?"
aliongea mkubwa wa Genge(MonNyeusi)
"hatukuwa na Jinsi Bosi maana sebastian aliweza kupigwa Risasi ya Mgongo"alijibu mfuasi mmoja wa monNyeusi.
"Haraka nendeni mkamtafute Sebastian kama atakuwa bado yuko hai muokoeni na mkishindwa muuweni kabisa mana yeye ni shahidi tosha atakaweza kutukamatisha sisi"
haraka haraka wafuasi watatu wa MonNyeusi na silaha zao walipanda pikipiki zao na kuelekea kumtafuta sebastian.
Itaendelea........................
0 comments:
Post a Comment
comment