CLEVER WEB TZ

Breaking News
Loading…

Pages

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
ENEZA BIASHARA YAKO

Friday, December 20, 2019

TYPHIN 04


TYPHIN 04
‘Hadithi ya kale, inayoishi’
HUSSEIN O. MOLITO
0718 97 56 59/ 0765 68 4870
“Kwa umuhimu wa hizi tafiti, siwezi kughaiiri mke wangu.”
“Basi jibu jepesi, tunaenda wote.”
Mke wa Mtafiti akaongea hayo na kumfanya Mr. Gibson kukosa pakutokea.
Wakarudi kwenye meza ya utafiti na kumuachia Samira majukumu ya Maabara hayo na wao wakaanza safari.
Safari ambayo imeleta madhara makubwa. Mr Gibson akasaidiwa akiwa taabani huku mke wake kipenzi akipotelea majini.
*******************
Inspekta Salim akakuna kichwa baada ya kuelezewa habari za msichana huyo anayefanya vitu vya ajabu mtaani tofauti kabisa na binaadamu wa kawaida. Alimuangalia Samira kwa sekunde kadhaa, kisha akanyanyuka.
“Naomba namba yako ya simu, nkihitaji kufahamu vitu vingine nitakutafuta. Ila kwa sasa nakuacha huru uendelee na ratiba zako.” Inspekta Salim akampatia Samira simu yake.
Baada ya Samira kuandika namba, Inspekta Salim akaihifadhi kwenye kitabu cha simu yake na kumruhusu Samira atoke.
Muda huo huo ile familia iliyokumbana na nguvu za kiumbe huyo, ikafika kituo cha polisi kuripoti.
“Kuna kiumbe ambaye si binaadamu wa kawaida, amesababisha uharibifu kwenye gari yetu.” Kijana huyo akafungua maelezo wakati Samira akikabidhiwa vitu vyake.
“Hebu ipange vizuri sentensi yako, maana utanichanganya wakati wa kuchukua maelezo yako. Huyo kiumbe aliyewashambulia, ni jinsia gani?” Askari akauliza na kuwatazama watu hao machoni.
“Ni msichana, tena anaonekana ni binti mdogo tu. Ana macho yanang’aa kama yapaka. Amevaa baibui lina urembo wa maua maua kwenye kifua.”
Kwa maelezo hayo tu, Samira akagundua kua watu hao walikua wakimzunguzia binti aliyesababisha kukamatwa kwake. Sasa akatega sikio ili aweze kujua amewafanya nini watu hao.
“ilikuaje mpaka akawasababishia ajali?” Askari akauliza tena huku akichukua faili la kesi kwa ajili ya kunakili hayo maelezo.
“Alikua anavuka barabara eneo ambalo halina kivuko. Nikapiga breki, ila gari ikasota kidogo kwakua nilikua spidi sitini. Chakushangaza binti huyo licha ya gari kumgusa, hakutikisika hata kidogo, aliniangalia tu kisha akaondoka. Ndipo tulipoenda kutazama gari yetu. Kama unavyoiona pale, ngao na bodi vyote vimebonyea. Utafikiri tumegonga mti.”
Maelezo hayo yalitosha kabisa kumfahamisha Samira kuwa yule msichana aliyemsaidia hakua binnaadamu. Hakutaka kuendelea kusikiliza. Akaamua kuondoka baada ya kuhakikisha vitu vyake vyote vipo sawa.
Akatoka nje na kuonana na dada yake, wakakumbatiana kwa furaha.
“kimekukumba kipi mdogo wangu?” Rabia akauliza.
“Twende nyumbani, hapa si pahala pazuri pakukaa.” Samira akaongea hayo na dada yake akaongoza kuelekea kwenye gari yake alipoegesha.
Walipokua njiani, simu ya Rabia ikaita na jina kwenye kioo cha simu likasomeka mama.
Wakaangaliana na kuamua kupokea.
“Asalaam aleykum.” Rabia akasalimia baada ya mawimbi ya sauti kuwaruhusu kuwasiliana.
“Aleykum salaam, ndo tunashuka hapa uwanja wa ndege, niambie mpo kituo gani ili tukodi gari mpaka huko?” Mama akaongea na kumfanya Rabia amuangalie mdogo wake.
“Njooni tu nyumbani kwa Samira, maana ameshaachiwa.” Rabia akaongea maneno hayo na kumfanya mama yake kushusha pumzi.
“Hebu mpe simu.” mama akaongea ili apate kuhakikisha.
Rabia akamkabidhi simu Samira.
“Binti yangu, pole kwa madhila ya Dunia.” mama akaongea kwa huruma baada ya kuhisi tu kuwa Samira ameshachukua simu.
“Nimeshapoa mama, kama mmekuja ni vyema tu mje kwangu. Haina haja ya kuongea mengi kwenye simu.” Samira akaongea na kumkatisha mama yake. Maana alifahamu kinachofuata hapo ni maswali mfululizo.
“Sawa Binti yangu, tunakuja.” mama yao akaridhika na kukata simu.
Rabia akamuangalia Samira na kutabasamu.
“katika watu wanaompatia mama yetu, ni wewe. Bi Mariam kwa kuongea tu, Alhamdulillah. Yaani ingelikua mimi hapa, hata nisingeweza kukwepa kuulizwa maswali yake.” Rabia akaongea hayo na kumfanya mdogo wake acheke.
“Mama anajua kua sipendi kuongea sana, napenda mtu adadavue shida yake kiufupi. Mambo ya kuonga na simu wee… hata sifagilii.” Samira akaongea hayo na kumfanya dada yake atabasamu tu.
Wakafika nyumbani na kutulia sebuleni. Nusu saa baadaye, wazazi wao wakafika na kuwapokea kwa furaha.
Wakumbatiana na kilichofuata hapo ni kuwasimulia mkasa mzima.
“Mungu mkubwa jamani. Huyo msichana siyo binadamu, naomba kuanzia leo hii, acha kuwakaribisha watu usiowafahamu. Ungeuliwa binti yangu endapo angehitaji kufanya hivyo.” Mama akaongea baada ya kuhadithiwa mkasa wa binti wa ajabu aliyekaribishwa na mtoto wake mpaka ndani.
“Ndo hivyo, Inspekta amechukua namba yangu kwa minajili ya kuwasaidia chochote pindi watakapokwama.” Samira akaongea na kulala kwenye mapaja ya mama yake.
“Kwahiyo binti yangu unapewa kazi ya upelelezi bila malipo.” baba aliyekua kimya muda wote, akaongea maneno yaliyofanya familia nzima iangue kicheko.
*********
Safari ya Mtafiti Gibson na mke wake Jada katika kuelekea baharini, ilianza kuingia doa toka hawajaianza safari hiyo.
Chombo kilisumbua kuwaka kwa muda mrefu na kuwafanya washangae. Maana ilichekiwa siku moja kabla. Kila kitu kilikua kipo sawa na hawakukitembeza chombo hicho baharini.
Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, ndipo chombo kilipowaka na wapendanao hao wakaanza safari.
Yaliwachukua msaa manne kwenye maji kufikia kwenye kina cha maji walichohitaji kufanya uchunguzi. Hapo wakasimamisha boti yao na kuchukua Vifaa mbalimbali vya kuoglelea na silaha pindi watakapokutana na dhoruba yoyote.
“Mke wangu itabidi ushike hii rada. Hizi rangi zina tafsiri kama utumiavyo barabarani. Ukiona kijani ujue nipo salama, ila ukiona nyekundu. Basi Piga bastola hii yenye baruti ya rangi juu kuomba msaada. Kwa hali yoyote ile,Tafadhali mke wangu, nakuomba usiingie kwenye maji.” Mtafiti Gibson akaongea hayo na kumkabidhi mke wake kifaa hicho.
“Subiri kwanza, kwanini hutaki niingie kwenye maji wakati mimi ni muogeleaji mzuri ?” Jada akauliza.
“Mke wangu, si kila kitu kinahitaji ubishi… unahitajika kuwa msikilizaji na kuamini ninapokuambia kua kuna kiumbe wa ajabu ameivamia bahari yetu. Na si samaki.” Mtafiti Gibson akaongea hayo na kumtazamamke wake usoni. Unyonge wake uliashiria kuridhika kishingo upande matakwa ya mume wake. Mr Gibson akamsogelea mke wake na kumkumbatia.
“Basi tumuite Junkle aje atusaidie, maana nina hofu ya kukupoteza mume wangu iwapo utakutana na viumbe vyenye nguvu kukushinda.” Jada akaongea na kumfaya Mtafiti Gibson amlaze mke wake kifuani.
“Usiwe na wasiwasi pindi Mtafiti Gibson akishindwa kupambana nao, maana hakuna kitu kitakachoshindikana pindi mume wako anapovaa cheo chake cha Agent Zero. Kiumbe chochote kitakachouinga huu mziki, Kitakufa.” Mr. Gibson akaongea hayo na kumtoa mke wake kifuani.
Kengele ya saa yake ya mkononi ikalia na kumfanya Mtafiti Gibson ashtuke sana. Maana saa yake iliweza kumuonesha vitu mbalimbali walivovitega kwenye maji.
“Kuna viumbe wengi wanakuja kwa kasi kutokea chini. Wapo usiwa wa boti yetu. Bila shaka wanakuja kutushambulia.” Mtafiti Gibson akaongea na kumuangalia mke wake aliyezidi kuingiwa na hofu.
“Sasa tunafanyaje mume wangu.” Jada akauliza huku akishika kichwa chake kama ishara ya kuchanganyikiwa.
“Nawamudu, acha nikapambane nao na kuchukua vipimo vyao vya damu. Nadhani itakua ni jamii ya viumbe vikorofi sana vya huku majini.”
Mtafiti Gibson akaongea hayo na kujitupa baharini.
Jada alikua akitetemeka huku macho yote yakiwa kwenye kifaa alichopewa. Kwa muda mrefu kifaa hicho kilisoma rangi ya kijani kuashiria kua mtafiti Gibson alikua salama.
Mara ghafla kifaa hicho kikaanza kupiga kelele na kubadilika rangu na kuwa nyekundu.
Jada akachanganyikiwa, akaichukua bastola iliyokua na fataki nyekundu na kupiga juu.
Hakukumbuka onyo alilopewa na mume wake juu ya tahadhari ya kutoingia majini, ila alihisi mue wake kwa muda huo alihitaji msaada wa haraka zaidi ya kuita boti zingine kutokea mbali.
Naye akavaa mtungi wa gesi na kuingia kwenye maji.
Alipata hofu kubwa baada ya kuona damu nyingi chini ya maji huku asimuone mume wake wala hao viumbe alivyokua akipambana navyo.
Baada ya kusogea zaidi chini ya maji, ndipo alipofanikiwa kuona viumbe wa ajabu wakipambana na Mtafiti Gibson.
Tukio la mke wake kuingia kwenye maji, likamfanya mtafiti Gibson ajaribu kumpa ishara atoke, ila kwenye maji ikawa ngumu ishara hizo kuonekana.
Wale viumbe wengine walipomuona Jada, wakamuacha Mtafiti Gibson aliyekua akiwajeruhi kwa silaha zake kali na kumfuata Jada ambaye silaha aliyoibeba haikua na uwezo wa kuwashinda viumbe hao waliokua na umbo la binaadamu lakini wenye mikia ya samaki.
Kucha ndefu, imara na uwezo wao wa kupambana wawapo kwenye maji, uliwafanya waupoteze uhai wa mke wa Mtafiti kwa sekunde chache tu.
Mtafiti Gibson akapata mtanziko wa nafsi baada ya kushuhdia tukio hilo. Maana yeye alikua na uwezo wa ziada zaidi ya binaadamu wa kawaida, hivyo aliweza kuwakabili viumbe hao na kile alichokihitaji kutoka kwao alishakipata. Kupigwa butwaa kwake baada ya kushuhudia mke wake akiraruriwa kwa makucha makali, kulimfanya apoteze nguvu ya kupambana na yeye kuanza kushambuliwa na viumbe hao wenye hasira.
Wengine walienda usawa wa boti na kuanza kuishambulia boti yao. Wakafanikiwa kuitoboa na boti hiyo ikaanza kuingiza maji.
Kengele ya saa ya Mtafiti Gibson ikalia kwa nguvu. Viumbe hao baada ya kusikia mlio huo, wakapiga kelele sana. Wakakimba na kupotea kwenye uso wa mtafiti Gibson.
Ghafla mfumo wa upumuaji kwa Mtafiti ukaanza kuwa mdogo. Alipoangalia mtungi wake wa hewa, ulikua umeshambuliwa kiasi cha kutokua msaada tena kwake.
Alizamia mita nyingi sana majini, bila tochi kubwa aliyovaa kichwani, ingelikua shida kuona chochote kwa umbali aliopo.
Aliogelea kwa spidi kubwa ili ajaribu kuokoa maisha yake. Maana kwa uwezo wa binaadamu wa kawaida, ni ngumu sana kuzuia pumzi zaidi ya dakika kumi uwapo kwenye maji.
Wakati huo msaada ulishafika na ndo walikua kwenye uchunguzi. Hata hivyo hawakufanikiwa kuona chochote kwakua mtafiti alikua mbali akipigania uhai wake.
Pumzi zilimshida mara kadhaa na kuruhusu kuingia mdomoni.
Mbali na uchovu, maumivu makali ya kushambuliwa na samaki hao wenye umbile la watu, akafanikiwa kufika juu akiwa hoi.
Akatamka neno moja tu, tena hakulimaliza. Akapoteza fahamu na kuanza kuzama tena.
Ikawa bahati, sauti yake ikasikiwa na askari wa kwenye maji na kuokolewa.
********
Jengo la Maabara lilikua tulivu, halina mtu yeyote ndani yake. Dokta Miley akaingia na kujifungia.
Akachuka ile sindano iliyokua na tafiti za Mr. Gibson na kuanza kuzichunguza.
Baada ya kuminya kimiminika hicho kwenye Test tube, akachukua kioo kidogo na kusambaza kimiminika hicho na kukiweka kwenye Microscope na kuanza kukichunguza.
Ilikua ni ajabu kutokea, maana kitu kilichomsomea kwenye mtambo huo hakuwahi kukutana nacho kabla.
“Anahitajika mtaalamu zaidi yangu ili aweze kusoma hivi vitu. Maana ni vigeni kwangu.” Doctor Miley akaongea baada ya kuambulia patupu.
Akachukua simu yake na kuandika namba kadhaa, kisha akapiga.
“Kaka, unaweza kuja Maabara maramoja?.” Dokta Miley akaongea baada ya siku yake kupokelewa.
“kuna nini ndugu yangu? maana najua huishiwi mipango.” Ikasikisa sauti upande wa pili.
“Nadhani ukiweza kutambuka ni kipi kimejificha kwenye tafiti zangu nilizonazo hapa Maabara, na sisi tutakua maarufu kama si matajiri wakubwa wa kuitikisa Afrika.” Dokta Miley akaongea maneno hayo na kumtia mshawasha mwenzake.
“Weeeh! Umegundua dawa ya kansa nini?” mwenzake akauliza kwa utani.
“We njoo… majibu yote utayapata huku.” Dokta Miley akaongea hayo na kukata simu. Akajikuta anatabasamu bila kujua kama mwenzake ataweza kumsomea ama naye atachemka kama yeye.
Haya! Dokta Miley ashaanza kujimilikisha zile tafiti za Mr. Gibson kabla muhusika hajafa. Hawafahamu kua hicho wanachokichunguza hakitoki kwa samaki wa kawaida. Bali na wale samaki wanye maumbile ya binaadamu kuanzia kiunoni kwenda juu.
Kipi Kitaendelea kwenye kigongo hiki? Ukumbuke ni TYPHIN, hadithi ya kale inayoishi!
Usisahau ku subscribe channel yangu youtube pindi utakapopitia hadithi hii inayopatikana huko kwa njia ya sauti.
kipindi cha NGOJA NICHEKE kinaruka kila ijumaa huko Youtube. Jina la account , Molito Brand
link ya kukupeleka Youtube ni hii chini!

0 comments:

Post a Comment

comment

PAKUA APP YETU

Kwa wale wapenzi wa Mziki Mzuri,filamu nzuri na Hadithi nzuri kutoka kwa waandishi mbalimbali, blog yetu ya Burudani, Tunapenda Kuwataarifu kuwa:

> Kama Hautumii App Basi tunakuomba PAKUA APP YETU MPYA HAPA Ili uweze Kupakua Nyimbo Mpya kirahisi
> Pia Utapata Taarifa kila wimbo Mpya unapotufikia.

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Official android App for www.cleverwebtz.blogspot.com

This application is developed with the following key features:
• Listening Music online with latest collection of tracks
• Download Music for listening offline
• Read story from different author
•watch movies online and download
• Listen to Music and do other things with a convenient way with playing background modes, customizable through the Notification bar (notification).

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Last Updates

DEREVA TOYO 14