Stori: Shabaha moja(One Target)
Mtunzi: ABiClever Yohlo
Sehemu:03
Tulipoishia>>haraka haraka wafuasi watatu wa MonNyeusi na silaha zao walipanda pikipiki zao na kuelekea kumtafuta sebastian.
Inaendelea>> "shit" alisema hivyo Ramso baada tu ya kuingia ndani ya kituo na kukuta miili ya askar wenzake ikibebwa na madakari kwaajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi lakin kati ya askar hao walio shambuliwa mmoja kati yao alikuwa bado yuko Hai na huyo pia alibebwa kwa ajili ya kwenda kupewa matibabu Ramso alibaki na mawazo.
"unadhani sebastian atakuwa hospital gani?"aliuliza mfuasi mmoja wa MonNyeusi aliyekuwa akiitwa Mad Lion Wakiwa mita kadhaa kutoka kwenye eneo la kituo.
"siumeona ile miili inapakiwa kwenye lile Gari la wagonjwa?"aliuliza Mad Kick nae pia ni mfuasi wa monNyeusi.
"Ndio nimeona"alijibu mad lion.
"basi tusubiri lile gari liondoke na Tuifuatilie inapo enda nina uhakika sebastian atakuwa huko"aliongea mad kick huku akipiga moto pikipiki.
Mad Lion na Mad Boy na wao pia walipiga moto pikipiki zao.
Ramso akiwa kwa mbali aliona zile pikipiki tatu zikilifuata gari la wagonjwa alipatwa na shaka kisha nayeye alichukua pikipiki yake na kuanza kufuatilia nyuma ya zile pikipiki za MonNyeusi.
Kwa bahati mbaya mfuasi mmoja wa monNyeusi aligundua kuwa kuna mtu anawafatilia.
"mnaona hiyo pikipiki nyuma mimi siielewi maana muda mwingi inatufatilia" aliongea mad Boy.
Hawakuzungumza cha ziada ila waliongeza speed ya pikipiki zao,na Ramso nae akaongeza speed ya pikipiki yake.
Ramso huku akiwa anaendesha pikipiki yake kwa speed aliingiza mkono kwenye mfuko wa shati lake kisha akatoa simu na kupiga kwa mkubwa wake.
"kuweni wa angalifu na huyo askari(Nikolasi) aliyejeruhiwa na risasi maana kuna watu wa tatu nimewaona wanafatilia gari ya wagonjwa iliyombeba nikolasi"aliongea Ramso kwa njia ya simu kisha akakata simu.
Wale wafuasi kipindi Ramso akiwa anawafatilia nyuma walifika njia ya Panda kisha walitawanyika kila mtu na barabara yake. Mmoja aliendelea kufuatilia nyuma gari la wagonjwa wengine wawili nao mmoja alienda kushoto mwengine kulia kwa makusudi ya kumchanganya Ramso.
Ila Ramso aliendelea kumfuata aliyekuwa anafuata gari la wagonjwa.
Baada ya muda kidogo wale wawili wakamzunguka Ramso na kutokea nyuma ya Ramso, na yule mmoja aliyekuwa mbele ya Ramso alisimamisha pikipiki kwa madoido na kumgeukia Ramso kisha akalenga shabaha zake kwenye Tairi la pikipiki ya Ramso, shabaha yake ilifanikiwa na kumuangusha Ramso,Ramso aliserereka mita amsini mbele na pale alipo kuweko mfuasi wa MonNyeusi aliekuwa mbele ya Ramso.
Ramso hali yake ilikuwa mbaya kwa kweli kisha wale wafuasi watatu wa MonNyeus walishuka kwenye pikipiki zao na kuanza kumsogelea Ramso Taratibu.
Kwa bahati nzuri na pia bahati mbaya kwa wale wafuasi wa MonNyeusi, Mkazi mmoja wa eneo hilo haraka akafuata simu yake ya mezani na kupiga simu Kituo Cha Polisi.
Ghafla ving'ora vya polisi vilisikika lakini wale wafuasi hawakuacha kumfuata Ramso.
Ramso alikuwa ameanguakiwa na makorokoro yaliyokuwepo eneo lile pikipiki yake ilipoishia kuserereka .
"polisi wanaakaribia eneo letu tufanyeni fasta kisha tuondoke" Mmoja kati ya wale wafusi aliongea kwa kuwasihi wenzake baada ya kuona ving'ora vya polisi vinalilia karibu sana na walipo wao.
Hawakupoteza muda wale wafuasi walipiga Risasi nyingi eneo lile alipokuwa Ramso. Kisha walipanda pikipiki zao na kuondoka.
******TUKIRUDI NYUMBANI KWA RAMSO********
ilikuwa ni saa kumi alifajiri "Ramso atakuwa ameenda wapi na mpaka sasa hajarudi"aliongea Jesi huku akiwa na wasiwasi.
Aliamua kuelekea Getini kumuuliza Mlinzi labda Ramso aliweza kumuaga.
"Dadaa Jesi mbona umeamka saa hizi?"aliuliza mlinzi wa Getini.
"embu acha maswali yako yasio kuwa na miguu wala kichwa embu nambie hivi Ramso wakati anatoka alikuaga?"aliongea jesi na kumuuliza mlinzi huyo.
"mmmh hakuweza kukuaga wewe waubani aniage mimi itakuwa maajabu"alijibu mlinzi.
Je akasema "sawa" kisha akaelekea kwenye ngazi ndogo ya kuingia ndani na akakaa kwenye ngazi hiyo na kushika kichwa huku akiwa ameinamisha kicha chake chini.
Itaendelea...................
Whatsapp Number +255624101615 Like my Page na Kisha share Tafadhali.

0 comments:
Post a Comment
comment