Friday, December 13, 2019
DEREVA TOYO 02
Dereva toyo Mtunzi:Richard Yassin Contact:0714137918 Sehemu ya 2 Hivyo nilipo ona amekwisha tulia barabara nilianza kuzichanga karata zangu ili niweze kuona angezipinduaje.Nachoshukuru ni kuwa tayari mlimbwende huyu sasa alikwisha anza kunielewa vema.Hivyo story zilinoga hadi tulipoingia maeneo ya Korogwe mahala ambapo tulipewa takribani dakika 10 kwa ajili ya kula.Siyo siri nilitamani mapaparazi wa ile kampuni ya ubashiri laiti kama wangelikuwepo wangepiga picha kwa ajili ya ukumbusho na kunogesha rasmi zoezi la upokeaji wa zawadi.Ila ndo hawakuwepo.Hivyo tuliposhuka katika gari kila mtu alishika kona yake katika banda analolipenda kwa ajili ya kupata chakula na kisha kurudi katika basi na safari kuendelea.Ila safari hii mambo yalikuwa ni moto haswaa kwani tulizidi kuzoeana kiasi cha hata kulishana kuku na nyama tulizokuwa tumebeba.Siyo siri kwangu ndo ilifika mahala pake kwani mara nyingi michezo kama hii niliipenda sana na hata kuvutiwa nayo.Nami sikuona aibu ya kumpa mahaba mazito ya mwambao wa pwani kwani mara nyingi watu hudharau na kusema ni mambo ya kizungu.Hatukujali macho ya watu kwani nilipokea chakula toka mdomoni kwake nami hakusita kupokea chakula toka mdomoni kwangu.Ili mradi mambo yalisogea mahala pake.Mara baada ya kumaliza kula,ilifika zamu ya soda ambako tulikuwa tukibadilishana mirija na kunyweshana soda zetu.Baadhi ya watu walitamani michezo yetu kwani mara nyingi kila kituko tulichofanya baadhi ya watu walikuwa wakipiga makofi ishara ya kuonyesha kwamba walifurahishwa nayo.Safari ya Dar es salaam ilikuwa mbali kwani mrembo huyu kutokana na shibe aliyokuwa nayo alipitiwa na usingizi nami kwa kuonyesha kumjali,nilimkumbatia na kuweka kichwa chake katika mapaja yangu ili alale vyema.Na kisha nikamfunika vizuri kama vile kuku anavyojali vifaranga wake pindi mvua inaponyesha au baridi inapopiga.Usingizi ulimpaa pale aliposikia konda anaita Chalinze."Oh! my God nimepitishwa.Kwani hapa ni wapi?"Alihoji dada huyo.Nilimuambia mahala tulipofikia.na kumuuliza kwani alihitaji kushuka wapi?"Ninashuka Kibaha kongowe."Alijibu mdada huyo nami nilimuahidi kumshtua pindi tutakapofika kituo chake.Kwa hiyo aendelee ku........Itaendelea!!!!
PAKUA APP YETU
Kwa wale wapenzi wa Mziki Mzuri,filamu nzuri na Hadithi nzuri kutoka kwa waandishi mbalimbali, blog yetu ya Burudani, Tunapenda Kuwataarifu kuwa:
> Kama Hautumii App Basi tunakuomba PAKUA APP YETU MPYA HAPA Ili uweze Kupakua Nyimbo Mpya kirahisi
> Pia Utapata Taarifa kila wimbo Mpya unapotufikia.
PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file
Official android App for www.cleverwebtz.blogspot.com
This application is developed with the following key features:
• Listening Music online with latest collection of tracks
• Download Music for listening offline
• Read story from different author
•watch movies online and download
• Listen to Music and do other things with a convenient way with playing background modes, customizable through the Notification bar (notification).
PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file








0 comments:
Post a Comment
comment