"Jesi ni nini unachowaza mbona umeshika Tama?"aliuliza Ramso kwa shauku ya kutaka kujua anachowaza jeska(jesi).
"Hapana nafikiria sana kuhusu siku yangu ya kuzaliwa ikifika nani atanifariji maana nimebaki yatima kwa sasa" alijibu jesi kwa unyonge sana uku akiendelea kushika tama na chozi likimdondoka jicho la kushoto.
"kweli inauma kutokuwa na wazazi ila mimi nipo jesi na usijali siku hiyo ikifika nina hakika utafurahia uwepo wangu" aliongea Ramso kwa upole ili angalau aweze kutuliza maumivu aliyo nayo Jesi kwa kuwakosa wazazi wake.
"asante ila ata sasa hivi nafurahia uwepo wako Ramso"
"Naapa nipo Tayar kuwa na wewe Bega kwa Bega kuhakikisha Tunalipa kisasi Cha wazazi wako"aliongea Ramso huku akiwa amekutanisha meno yake kwa uchungu.
************MWAKA MMOJA NYUMA*************
ilikuwa ni usiku wa furaha katika Familia ya Bwana Stephano.
"Mwanangu Jeska nakupenda sana na napenda sana kukuona unasoma na kutimiza malengo yako niko tayari kufanya lolote ili mwanangu uweze kuendelea na masomo yako ya Chuo, nimeuza nyumba yangu ile Nyingine ili niweze kupata fedha za kukulipia ada mwanangu" aliongea bwana Stephano.
Ghafla mlio wa Risasi ulisikika mlangoni mwa Nyumba ya Bwana stephano na Mlango ulipigwa teke moja kwa moja watu wanne walio ziba nyuso zao kwa vinyago waliingia ndani na bila ya kuuliza walimpiga Risasi ya ziwa la kushoto Mama Jesi na Kisha walifuata kwa bwana stephano nae pia walimuua kinyama kwa kumchinja shingo. Ving'ora vya Gari za polisi na gari ya kubebea wagonja vilisikika hapo jesi akapata pengo na kuponyoka kwenye mikono ya watu hao.
Baada ya muda kidogo Gari za polisi na Gari la wagonjwa zilifika eneo la Tukio, askari mkuku mkuku walingia ndani kwenye nyumba ya Tukio, askari walitafuta huku na kule hawakuona watu wala mtu zaidi ya zile maiti mbili .
Polisi mmoja aliye fahamika kwa Jina la Ramso alielekea eneo la msalani kwa ajili ya kugagua,huko alikuta mlango umefungwa kwa ndani alipiga teke mlango ule na kumkuta Jesi amejikunyata pembeni kabisa
alimsogelea na Kumuonyesha kitambulisho Jesi ili kumtoa wasi wasi alionao kisha akamshika mkono na Kumtoa Nje kabisa na kisha alimwambia aingie kwenye gari la wagonja, Jesi aliingia ila Baada ya kuingia tu alipoteza Fahamu.
******TUNARUDI MWAKA WA SASA**************
"sawa Ramso wacha mimi niende Chumbani kupumzika kidogo" aliongea Jesi huku akielekea chumbani kwake.
Itaendelea...........................
0 comments:
Post a Comment
comment