CLEVER WEB TZ

Breaking News
Loading…

Pages

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
ENEZA BIASHARA YAKO

Tuesday, November 26, 2019

BROTHERHOOD (UKAKA) 2


BrotherHood(2)
Mtunzi:Abi
Tulipoishia>>"Baba mzigo ulifika salama ila baadhi ya vijana wetu wamekamatwa na jeshi la polisi"aliongea Jacob.
"Huo ni uzembe mwanangu je wamekamatwa vijana wangapi?" aliongea chris<<
Inaendelea>>"nisamehe baba,wamekamatwa vijana watatu ambao ni Gilbert,Moslin na Timeka"aliongea Jacob kwa upole sana.
"Hahahaha Jacob umekua mpole sana, usijali huo ni mpango wangu"aliongea Chris.
"Unamaanisha nini kusema hivyo baba"aliuliza Jacob akionekana amebaki njia ya panda kwa maneno ya chris.
"Unakumbuka niliwaambia mgawane vikundi na kila kundi lipite njia yao" aliongea Chris kwa njia ya swali kwa lengo la kutaka kumpa maana Jacob.
"Ndio nakumbuka baba"alijibu Jacob kwa shauku ya kutaka kujua maana ya baba yake.
"Unajua mkubwa wa kikundi cha MadDragons ameungana na sisi lakini sio kwa lengo zuri"aliongea Chris.
Jacob akadakia kati kwa kuuliza"una maana gani?"
"usiwe na haraka jacob utaelewa, na wale vijana ni wa kundi hilo kwa niliwachoma kwenye jeshi la polisi ili kummaliza mkubwa wa kundi hilo"aliongea Chris Huku akitabasamu.
**UPANDE WA JUSTIN NA MAMA YAKE**
"Acha kuwaza sana mama,alaf mama unakumbuka kama leo ni siku yako ya kuzaliwa nahitaji tutoke" aliongea Justin akimuangalia mama yake kwa macho ya upendo.
"Ndio wew unanikumbusha sasa hivi"aliongea Jackline.
"Sawa mama basi kajiandae tutoke mimi namalizia kula pia nikajiandae"aliongea Justin.
**UPANDE WA MKUBWA WA KIKUNDI CHA MADDRAGON**
"Bosi nimepokea simu kutoka kwa Chris ,anasema kuwa baadhi ya vijana walikamatwa kwenye ule mpango na walio kamatwa ni vijana wa kundi letu"aliongea Mfuasi wa kundi la Maddragon anayefahamika kwa jina la Stanley.
"Nina wasiwasi huo utakuwa ni mpango wa Chris, na kama ni kweli itakuwa tayari ameshangundua Tulicho kipanga juu yake na kama amejua basi itakuwa kuna msaliti katika kundi letu"aliongea mkubwa wa kundi hilo anafahamika kwa jina la Gerrard.
**KITUO CHA POLISI**
Polisi mmoja alielekea sehemu ya kupiga simu ili kumpa taarifa Justin "Halloo mkuu,hawa wahalifu tumewabana mpaka mmoja wao amekubali kumtaja kiongozi wao".
"Sawa nitafika hapo sasa hivi"aliongea Justin kumjibu polisi huyo kwa njia ya simu.
**UPANDE WA JUSTIN**
"Mama samahani naomba nikurudishe nyumbani nahitaji kwenda kazini"aliongea Justin
"usijali mwanangu"aliongea Jackline .
Kisha wakatoka walipo kuwepo na kuelekea lilipo gari lao.
Wakati wanaelekea kwenye gari Ghafla mlio wa risasi ukasikika "PAaaaaaaaaa" mdogo mdogo Jackline akaanguka chini.
Justin bila ya kupoteza muda akachomoa bastola ndogo na kujibu mashambulizi kisha alim'buruza mama yake kipole pole mpaka kwenye ukuta .
punde si punde vilisikika ving'ora vya gari za polisi.
Kikosi cha maadui kilipo sikia hivyo wakaamua kuondoka eneo hilo.
"vipi uko salama mkuu"aliuliza askari mmoja ambaye ni rafiki pia wa karibu wa Justin anafahamika kwa jina David.
"ndio ,ila nisaidie kuita gari la wagonjwa"aliongea Jacob kumsihi David aite gari la huduma ya kwanza(ambulance).
0623892880/0654445214
ITAENDELEA..........

0 comments:

Post a Comment

comment

PAKUA APP YETU

Kwa wale wapenzi wa Mziki Mzuri,filamu nzuri na Hadithi nzuri kutoka kwa waandishi mbalimbali, blog yetu ya Burudani, Tunapenda Kuwataarifu kuwa:

> Kama Hautumii App Basi tunakuomba PAKUA APP YETU MPYA HAPA Ili uweze Kupakua Nyimbo Mpya kirahisi
> Pia Utapata Taarifa kila wimbo Mpya unapotufikia.

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Official android App for www.cleverwebtz.blogspot.com

This application is developed with the following key features:
• Listening Music online with latest collection of tracks
• Download Music for listening offline
• Read story from different author
•watch movies online and download
• Listen to Music and do other things with a convenient way with playing background modes, customizable through the Notification bar (notification).

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Last Updates

DEREVA TOYO 14