CLEVER WEB TZ

Breaking News
Loading…

Pages

TANGAZA NASI

TANGAZA NASI
ENEZA BIASHARA YAKO

Sunday, November 24, 2019

BROTHERHOOD (UKAKA)


COPIED PICTURE IF UR THE OWNER CONTACT ME abicleverjunior@gmail.com


Stori: BrotherHood(Ukaka)
Sehemu Ya:1
Mtunzi:Abiclever Yohlo
Mnamo mwaka wa 2000/2/23 majira ya saa 5asubuhi katika bustani ya Nyumba moja ya Tajiri kulikuwa na watoto wawili wa kiume mmoja alifahamika kwa jina la justin na mwengine alifahamika kwa jina la jacob watoto hao walikuwa wakicheza katika mabembea ya nyumba hiyo.
Ghafla ikasikika sauti ya kike ikiwaita, watoto hao waligeuza macho na kuangalia kule iliposikika hiyo sauti.
''Mamii''waliita watoto hao kwa furaha iliyo pitiliza.
kabla watoto hao wajafika kwa mama yao ilisikika sauti nzito "Jackline umefuata nini kwenye nyumba Yangu?" Aliongea Chris Baba wa watoto hao wawili.
"Nimekuja kuwachukua watoto wangu"aliongea Jackline mama wa watoto hao.
"Unataka kuwachukua watoto wangu uwapeleke wapi?"aliongea chris kwa Jazba sana.
"Haikuhusu ujue wapi nawapeleka hawa ni watoto wangu"aliongea Jackline bila ya hofu ya aina yoyote.
"Mlinzi njoo utoe hii taka taka hapa na nisiione tena humu ndani"aliongea chris kumuita mlinzi aje kumtoa jackline.
"Wala usijali naondoka mwenyewe ila nitarudi tena, Kwaherini wanangu nitarudi"aliongea jackline na akaelekea getini.
Jioni ya siku hiyo Chris alipata barua yenye ujumbe kuwa anahitajika mahakamani kesho asubuhi kwa ajili ya kesi ya watoto.
Siku iliyofuata Chris alifika mahakamani,na jackline pia alifika mahakamani.
Saa kazaa zilipita baada ya mahakama kuridhika na maelezo ya pande zote mbili hivyo iliamua kuwa Mama amchukue mtoto mdogo ambaye ni justin na Baba amchukue mtoto mkubwa ambaye ni Jacob.
Japo ilikuwa ngumu kwa pande zote mbili lakini hakukuwa na jinsi hivyo Jackline alienda nyumbani kwa Chris na kumchukua Justin na kwenda kuishi nje kidogo ya mji huo.
*BAADA YA MIAKA 15*
"Mpango huu umeenda sawa kesho tunahitajika kuingia katika mpango mwingine ila na hawa wahalifu tulio wakamata ni lazima tuwabane mpaka waseme ni nani bosi wao" aliongea justin akiwa amevaa mavazi ya Jeshi la polisi na alikuwa ni askari mwenye nyota tatu.
"sawa mkuu"walijibu askari wengine ishara kuwa wamekubaliana na Justin.
Baada ya muda Justin alirejea Nyumbani.
"Mamaaa nimerudi"aliongea Justin Kumjulisha mama yake.
"Sawa mwanangu ila je unajua kama najivunia sana mafanikio yako mwanangu lakini sijui kaka yako anaendelea vipi"aliongea Jackline.
"Baba mzigo ulifika salama ila baadhi ya vijana wetu wamekamatwa na jeshi la polisi"aliongea Jacob.
"Huo ni uzembe mwanangu je wamekamatwa vijana wangapi ?"aliuliza Chris.
0624101615
ITAENDELEA......................

0 comments:

Post a Comment

comment

PAKUA APP YETU

Kwa wale wapenzi wa Mziki Mzuri,filamu nzuri na Hadithi nzuri kutoka kwa waandishi mbalimbali, blog yetu ya Burudani, Tunapenda Kuwataarifu kuwa:

> Kama Hautumii App Basi tunakuomba PAKUA APP YETU MPYA HAPA Ili uweze Kupakua Nyimbo Mpya kirahisi
> Pia Utapata Taarifa kila wimbo Mpya unapotufikia.

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Official android App for www.cleverwebtz.blogspot.com

This application is developed with the following key features:
• Listening Music online with latest collection of tracks
• Download Music for listening offline
• Read story from different author
•watch movies online and download
• Listen to Music and do other things with a convenient way with playing background modes, customizable through the Notification bar (notification).

PAKUA APP YETU MPYA HAPA
BONYEZA HAPA>http://www.mediafire.com/file/qtoi8pn4bj4dqct/Cleverwebtz.apk/file

Last Updates

DEREVA TOYO 14